![]() |
| RAIS SAMIA SULUHU HASSANI |
Mwandishi wetu, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Rais wa Jamuhuri ya Muungano, Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua mkutano wa sita wa kuongeza uhamasishaji katika masuala ya usawa wa kijinsia haki na ustawi wa wasichana na wanawake katika nyanja zote Women Deliver Conference ambao kwa mara ya kwanza unafanyika barani Afrika nchini Rwanda na kuhusisha wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika Kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambapo mitandao kadhaa imeundwa mikoani.
Miongoni mwa mitandao hiyo ni Mtandao wa kukabiliana na ukatili dhidhi ya wanawake na watoto kwa Jamii za pembezoni (CAIC -Tanzania) ambao umeundwa na Mashirika 10 ikiwepo shirika la MIMUTIE WOMEN ORGANIZATION na shirika la waandishi wa habari wanaosaidia jamii za pembezoni (MAIPAC)
Waziri wa Maendeleo ya Jamii , jinsia, wanawake na makundi maalum Dr. Dorothy Gwajima akizungumza na waandishi wa Habari amesema mkutano huo utafanyika katika jiji la Kigali, Rwanda kuanzia tarehe 17 hadi 20 Julai mwaka huu.
Waziri huyo wa Maendeleo ya Jamii , jinsia, wanawake na makundi maalum ndiye atamwakilisha Mheshimiwa Rais katika mkutano huo nchini Rwanda.
Amesema Mkutano huo utaleta pamoja wanawake katika ngazi ya jamii, asasi za kiraia, wanaharakati vijana, serikali na wadau wa maendeleo kubadilishana uzoefu na kujadili hatua muhimu zinazohitajika ili kuendeleza haki za ardhi za wanawake, mazingira, masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na masuala ya afya.
“Watoa mada watajadili jinsi haki na milki salama za ardhi za wanawake zilivyo na nyenzo ya kuendeleza usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu kwa kutatua migogoro, kukabiliana na majanga ya mara kwa mara, na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi , usalama wa chakula na umaskini"
Mashirika kadhaa ya nchini Tanzania na nchi nyingine Duniani yanatarajiwa kushiriki mkutano huo.


No comments:
Post a Comment