SIKUPIGA KURA KUBINAFSISHWA BANDARI - OLE SENDEKA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 21 July 2023

SIKUPIGA KURA KUBINAFSISHWA BANDARI - OLE SENDEKA

 

Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka, akizungumza kwenye kikao cha baraza la jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) cha wilaya hiyo, kilichofanyika mji mdogo wa Mirerani.

Na Mwandishi wetu, Simanjiro 


maipacarusha20@gmail.com


MBUNGE wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka, amesema yeye binafsi hakukubaliana na uwekezaji wa bandari kwa Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World na hakupiga kura hata Bungeni.


Ole Sendeka ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Simanjiro kilichofanyika katika ukumbi wa Panama, Mji mdogo wa Mirerani.


Amesema yeye binafsi hakufurahishwa na ubinafsishwaji wa bandari kupitia Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World, hivyo hakuunga mkono hata kwenye tukio la upigaji kura bungeni hakushiriki.


“Awali, niliwaambia kwenye kikao cha wabunge wa CCM kuwa siungi mkono suala la ubinafsishaji wa bandari ya Dar es salaam na hata bungeni sikupiga kura niliondoka ili nisiwepo,” amesema Ole Sendeka.


Mkazi wa mji mdogo wa Mirerani, Seleman Issa amesema hamuungi mkono mbunge kwa kuzungumza hadharani kuwa anapinga ubinafsishaji wa bandari ya Dar es salaam, kwani wapiga kura hao watasambaza habari kuwa Ole Sendeka hataki ubinafsishaji bandarini.


“Huyo mbunge siyo ajabu hata bandarini hajawahi kufika wala bwawa la Kidawash lipo kwenye kata ya Shambarai Wilayani Simanjiro, hajawahi kufika na wala hajui hasara tunayopata kwani awali bandari ya Dar es salaam siilikuwa imebinafsishwa au sababu hao ni waarabu siyo waswahili,” amesema.


Mkazi wa mtaa wa Zaire Haji Mshamu amesema gati 0 hadi 7 eneo ambalo Tanzania imeingia mkataba wa makubaliano na Serikali ya Dubai kwa ajili ya uendashaji kupitia kampuni ya DP World utakuwa na manufaa kwa nchi.


Haji amesema uwekezaji huo ni mzuzri kwani hivi sasa bandari ya Dar es salaam inachangia mapato ya serikali kwa asilimia 36 hadi 40 kwa shilingi trilioni 7 kwa mwaka.


Amesema mwekezaji DP World akipewa eneo hilo ili afanye kazi mapato yataongezeka hadi shilingi trilioni 26 ambapo bandari hiyo itachangia mapato yote ya Serikali kwa asilimia 67 ya mapato yote ya Serikali.



No comments: