UVCCM SIMANJIRO WAFANYA KIKAO CHA BARAZA MIRERANI NA KUGAWA KADI KWA WANACHAMA WAPYA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 3 July 2023

UVCCM SIMANJIRO WAFANYA KIKAO CHA BARAZA MIRERANI NA KUGAWA KADI KWA WANACHAMA WAPYA

 




Na Mwandishi wetu, Mirerani


maipacarusha20@gmail.com


JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamefanya kikao chao cha Baraza kwenye Mji mdogo wa Mirerani kikiongozwa na Mwenyekiti wake Timothy Ngoyay Mollel.


Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Manyara, Inyasi Amsi, mbaraza wa UVCCM Taifa wa Mkoa wa Manyara, wakili msomi Christine Millya, Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka na Mbunge wa Viti maalum Vijana Taifa, kupitia Mkoa wa Manyara, Asia Halamga.


Pia, wenyeviti wa UVCCM wa wilaya nne, Hamza Mngia (Kiteto), Elisante Shauri (Mbulu), Justin Ammi (Hanang') na Solomon Mpaki (Babati vijiji) wameshiriki kikao cha baraza hilo.


Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Simanjiro, Timothy Ngoyay Mollel akizungumza kwenye kikao hicho cha baraza la UVCCM Wilaya hiyo amewapongeza wajumbe na viongozi walioshiriki na kuwaunga mkono.


Mollel amesema agenda kubwa ya baraza lao ilikuwa kumpitisha Katibu Hamasa na Chipukizi wa Wilaya hiyo, Comrade Matei Damas Siria, uzinduzi wa shina tawi la Songambele 'Kona ya Dagaa' na kupokea taarifa ya kamati ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa UVCCM wa wilaya.


Amesema pia wamegawa kadi kwa wanachama wapya na vijana kupaza sauti zao kwa mbunge ili awapambanie kupata ajira katika kampuni ya Franone Mining LTD na maeneo mengine.


"Nawapongeza wajumbe wote waliohudhuria kikao hiki cha Baraza la UVCCM la Wilaya ya Simanjiro na wageni wote waalikwa mliofika kutupa joto katika kikao chetu," amesema Mollel.


Katibu wa UVCCM Wilaya ya Simanjiro, Azizi Risasi amewapongeza wajumbe wote wa Kata mbalimbali za Simanjiro waliojitokeza na kuhudhuria kikao hicho cha baraza.


Katibu Hamasa na Chipukizi wa Wilaya ya Simanjiro, Comrade Matei Damas Siria amewashukuru wajumbe hao kwa kupitisha kwa kishindo jina lake mara baada ya kufikishwa kwa wajumbe wa kikao hicho.


Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Manyara, Inyasi Amsi amewapongeza viongozi wa UVCCM Wilaya ya Simanjiro kwa kufanikisha kufanya kikao chao cha baraza lao.


Mwenyekiti mstaafu wa UVCCM Mkoa wa Manyara, Mosses Method Komba amewatakia kila la heri viongozi wote wapya wa UVCCM wa mkoa huo katika kutimiza majukumu yao mapya.



No comments: