WAZIRI MCHENGERWA ATAKA WANANCHI KUUNGA SERIKALI INAFANYA MAKUBWA KULETA MAENDELEO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 16 July 2023

WAZIRI MCHENGERWA ATAKA WANANCHI KUUNGA SERIKALI INAFANYA MAKUBWA KULETA MAENDELEO

 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia Mkoa wa Pwani na Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa

Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa Kibiti


Na: Mwandishi wetu, Pwani


maipacarusha20@gmail.com


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia  Mkoa wa Pwani na Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema wananchi wanatakiwa  kulinda amani iliyoletwa na Serikali ya CCM   kwa  kuwa ndiyo muhimili pekee  wa kuwaletea  maendeleo.


Akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa CCM, Wilaya Kibiti  leo  mjini  hapo ambao Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,   Abdulrahman Kinana  amekuwa  Mgeni Rasmi ambapo amesisitiza kuwa  Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa  ya  kulinda  amani  katika kipindi cha awamu zote hivyo  hawana sababu ya  kuhangaika  kuchagua  viongozi wa vyama vya upinzani.


Aidha, amefafanua kuwa Serikali  ya awamu hii chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya  kazi kubwa  ya kuwaletea maendeleo wananchi wake na kwamba    maendeleo hayo  yamefanyika kila kona ya Tanzania katika  kipindi kifupi cha miaka miwili.


Mkutano huo maalum wa Wilaya ya Kibiti  ulikuwa na ajenda ya kuwasilisha  utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 kwa kipindi cha Oktoba 2020 hadi Juni 2023 wa miradi ya Maendeleo yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 32 katika  wilaya hiyo.


Akizungumzia kuhusu jimbo lake la Rufiji,  Mchengerwa amesema anamshukuru Rais Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha za  maendeleo ambazo zimeleta mapinduzi makubwa kwenye sekta zote kuanzia uboreshwaji wa miundombinu ya  barabara, sekta ya elimu, Afya na kilimo.



Amesema  mkakati wa sasa  ni  kuwaleta wawekezaji  ili waje kuwekeza katika  miradi mbalimbali  katika  jimbo  hilo hususan  kwenye eneo  la ujenzi wa  mahoteli na  zoo  kwa ajili ya kufugia Wanyama kwa kuzingatia kuwa ukanda huu ni miongoni mwa kanda  zenye Wanyama wengi wa porini.


Ametoa wito kwa wawekezaji kuja  kuyatambua maeneo ya uwekezaji na  kuwekeza ambapo  pia amefafanua  kwamba  anatarajia kuendelea kufanya  onesho kubwa desemba mwaka huu la kumuenzi mwanasiasa Mkongwe hayati Bibi Titi Mohamed ambalo mbali na kuelezea  historia  ya wanarufiji litatumika kutangaza  viovutio na fursa za uwekezaji katika wilaya ya Rufiji.


Makamu Mwenyekiti Komred Kinana  amempongeza   Mchengerwa  kwa  kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya kama  Mbunge na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa mkoa wa Pwani. 


Aidha, amesifu kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea watanzania maendeleo katika kipindi kifupi ambapo amefafanua  kuwa  inatokana na  mahusiano mazuri aliyoyajenga na mataifa mbalimbali  duniani. Amewaomba watanzania  kuiendelea kumwombea


Amesema hii ndiyo awamu pekee ambayo  Serikali  imepata  fedha nyingi za  ufadhili na kwamba katika kipindi hiki Serikali imefanya  ujenzi  mkubwa wa  miundombinu  ikiwa ni pamoja na madarasa na zahanati.



No comments: