WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA 47 YA SABASABA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 14 July 2023

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA 47 YA SABASABA

 






Na Mwandishi wetu


maipacarusha20@gmail.com


Wizara ya Maliasili na Utalii imeibuka Kidedea kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) Jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa tuzo na Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ally Mwinyi ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa Maonesho hayo. 


Akielezea Tuzo hiyo ya 

Banda bora na mashuhuri category ya Wizara na Taasisi, Mwenyekiti wa Maonesho ya Saba Saba Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Filex John, amesema ni Matokeo chanya ya Uongozi mzuri wa Wizara hiyo pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na Watumishi wa Wizara hiyo ya utoaji huduma kwa Kiwango cha juu kwa wote waliofika kwenye Banda hilo. 


Bw. John amewashukuru wadau na wananchi wote waliojitokeza kupata huduma kwenye Banda hilo la Maliasili, pamoja na ushirikiano waliotoa katika kuhakikisha Maonesho hayo yanakuwa na Mafanikio Makubwa.

No comments: