Dokta Abbas aipa kazi TAWIRI kusaidia mbinu Bora kuendeleza uhifadhi nchini - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 18 August 2023

Dokta Abbas aipa kazi TAWIRI kusaidia mbinu Bora kuendeleza uhifadhi nchini

 




Na Mwandishi Wetu, 


maipacarusha20@gmail.com


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.Dk Hassan Abbas ameitaka taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori nchini(TAWIRI) kutoa mbinu Bora zitakazowezesha uhifadhi na ustawi wanyamapori .



Akizungumza na menejimenti ya taasisi  hiyo , Dkt. Abbas amesema kipaumbele cha  Wizara ya  Maliasili na Utalii  ni  kuendelea  kuhifadhi maliasili iliyopo  kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.


Amesema sekta ya uhifadhi nchini inaitegemea  TAWIRI  kutoa mbinu bora zitakazo wezesha uhifadhi na ustawi wa wanyamapori na makazi yao.


Dkt. Abbas ametoa wito kwa  Viongozi wa TAWIRI kuhakikisha  umma unapata matokeo ya Tafiti za wanyamapori  zinazofanyika  ili kuzitumia kwa maendeleo.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Dkt. Ernest Mjingo  amemshukuru Katibu Mkuu kwa ziara na nakuahidi kutekeleza maelekezo yote kwa manufa ya uhifadhi nchini.

No comments: