Kesi ya mtuhumiwa wa Ujangili wa Twiga yaanza kuunguruma Babati - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 15 August 2023

Kesi ya mtuhumiwa wa Ujangili wa Twiga yaanza kuunguruma Babati



Mwandishi wetu,Babati


maipacarusha20@gmail.com


Mahakama ya Hakimu Mkazi Babati, mkoa wa Manyara, imepokea kielelezo cha simu ya mkononi ya mtuhumiwa wa ujangili wa Twiga, Amos Benard maarufu kama Meja, katika kesi ya uhujumu uchumi ambayo inamkabili.


Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Victor Kimario alipokea kilelezo hicho cha simu, ambacho kiliwasilishwa mahakamani na shahidi wa kwanza wa mashitaka, Afisa Wanyamapori Emmanuel Bayo  ambaye ndiye alihusika kumkamata mtuhumiwa huyo.


Kielelezo hicho, kilikuwa na ujumbe wa simu ambao umetumwa kwa watu mbali mbali, wakitaarifiwa kuuzwa kwa nyama ya Twiga. 


Hakimu Kimario pia alipokea vielelezo vingine hati ya ukamataji na hati ya makabidhiano ya vitu ambavyo alikamatwa navyo mtuhumiwa huyo.


Shahidi huyo, akiongozwa na waendesha mashitaka wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori(TAWA),Getrude  Kariongi na Shahidu Kajwangya, waliomba mahakama kupokea vielelezo hivyo, kama sehemu ya ushahidi.


Hata hivyo, Mtuhumiwa huyo baada ya kuulizwa na Hakimu Kimario kama anapingamizi la  mahakama kupokea vielelezo hivyo alieleza hana pingamizi.


Awali, Mwendesha mashitaka  Kariongi alieleza mahakama kuwa, Mtuhumiwa huyo, anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi  baada ya kukamatwa na nyara za serikali kinyume sha sheria April 22, mwaka huu, kijiji cha vilima vitatu ndani ya Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge.


Kariongi alisema mtuhumiwa huyo, pia anakabiliwa na shitaka la makosa ya mtandao, kutokana na kumiliki simu ambayo namba yake haijasajiliwa kwa jina lake.


Kesi hiyo, inatarajiwa kuendelea kusikilizwa Agosti 21,mwaka huu, ambapo mashahidi wengine wataendelea kutoa ushihidi wao na mtuhumiwa amerudishwa mahabusu.

No comments: