LINDI KUMEKUCHA, MAONYESHO YA MADINI, TAMASHA NA FURSA ZA UWEKEZAJI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 17 August 2023

LINDI KUMEKUCHA, MAONYESHO YA MADINI, TAMASHA NA FURSA ZA UWEKEZAJI

 

Katibu Tawala wa mkoa wa Lindi, (RAS) Zuwena Omary Jiri


Na Mwandishi wetu, Lindi 


MKOA wa Lindi unatarajia kufanya maonyesho ya madini na fursa za uwekezaji yatakayohusisha wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.


Mkoa wa Lindi yanapatikana na kuchimbwa madini ya aina mbalimbali ikiwemo dhahabu, nickel, ganeti ya kijani, manganese ore, marble, gypsum na ulanga (kinywe).


Katibu Tawala wa mkoa wa Lindi, (RAS) Zuwena Omary Jiri amesema maonyesho hayo yatafanyika kwa muda wa siku sita wilayani Ruangwa Agosti 21 hadi 26.


RAS Zuwena amesema tamasha na maonyesho hayo yatahusisha fursa mbalimbali zinazopatikana mkoani Lindi ikiwemo madini, utalii, kilimo, mifugo na uvuvi.


"Lengo ni kuangazia fursa zilizopo mkoani Lindi na kujenga jukwaa ambalo wadau wa sekta ya madini na sekta shirikishi watapata nafasi ya kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kutangaza fursa zilizopo mkoani Lindi," amesema RAS Zuwena.


Amesema wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wafanyabiashara, wawekezaji na wapenda maendeleo tofauti kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki tamasha na maonyesho hayo.


Amesema kauli mbiu ya maonyesho hayo ni wekeza Lindi kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya jamii.


No comments: