Mbunge wa Uingereza Tracey Crouch apata furaha tele kufika kileleni Mlima Kilimanjaro - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 5 August 2023

Mbunge wa Uingereza Tracey Crouch apata furaha tele kufika kileleni Mlima Kilimanjaro

 





Na: Mwandishi wetu,

maipacarusha20@gmail.com


 Mbunge  wa Bunge la Uingereza, Tracey  Crouch na wenzake amefanikiwa kufika kileleni Mlima Kilimanjaro akiwa katika kampeni ya kuchangisha fedha ili kugharamia matibabu ya Kansa ya matiti kwa wanawake.


 Crouch anapanda   Mlima Kilimanjaro,akiwa na wanawake wenzake wanane kupitia kampuni ya Big Expedition and Safaris ya jijini Arusha na Agosti 5 anatarajiwa kupokewa Mweka.

 


Crouch ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Michezo wa Uingereza kati ya mwaka 2017/18  alifika kileleni akiwa na furaha kubwa ya kupanda Mlima Kilimanjaro.


Mbunge huyo amekuja nchini kupitia kampuni ya kimataifa ya Utalii ya Uingereza ya Action Challenge  kwa kushirikiana na Big Expedition and Safaris 


safari ya kupanda Mlima huo, iliyoanza Julai 29,2023 ilipewa jina la Delux VIP  na alikuwa akisaidiwa na timu ya wasaidizi 55.


 

Mkurugenzi wa kampuni ya Big Expedition and Safaris, Angel Minja akizungumza na MAIPAC media amesema kampuni hiyo inampongeza mbunge huyo kufika kileleni .


"Tunampongeza ametimiza lengo si kazi rahisi kupanda Mlima Kilimanjaro na kufika kileleni"amesema


Amesema mbunge huyo atapokelewa eneo la Mweka kwa shangwe kubwa kwani ametimiza lengo na atakuwa Balozi mzuri wa Mlima Kilimanjaro.



         

No comments: