
Na: Mwandishi WETU, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Hamsini amepiga marufuku upimaji wa magari yanayotoka viwandani kupeleka mizigo katika maghara ya vindandani ya ndani ya Jiji hilo kama ilivyo kuwa awali ambapo utaratibu uliwekwa na mtangulizi wake Dkt John Pima.
![]() |
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Hamsini akizungumza na waandishi wa habari |
Ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kufuatia malalamiko yaliyotelewa na wafanyabiashara hao Jijini Arusha mbele ya Waziri wa Viwanda na biashara Dkt, Ashatu Kijaji alipo kutana na wafanya biashara na wawekezaji wa Mkoa wa Arusha kwa lengo la kusikiza kero zao na changamoto zinazo wakabili.
Hamsini ameeleza kuwa Halmashauri hiyo imesitisha upimaji wa magari yote yanayobeba mizigo inayotoka viwandani au Maghalani na kusambazwa ndani ya Jiji la Arusha kama ilivyo kuwa hivyo awali.
"Tumepokea malalamiko kutoka kwa wafanya biashara kwamba kuna tabia iliyo jitokeza ya kulazimisha magari yanayo beba kutoka viwandani Arusha na kwenda maeneo ya ndani ya jiji letu la Arusha kwenda kupima katika mizani ya ngarenaro ambayo inaendeshwa na kampuni ya Raki Bridge kwa ushirikiano na halmashauri ya jiji la Arusha". Amesema Hamsin.
"Napenda kumuelekeza Meneja wa Raki Bridge kuwa magari yote yanapo pakia na kushusha bila kutoa nje ya mipaka ya jiji la Arusha hayalazimiki kupima uzito kwenye mizani yako yanapo kuwa yamebeba bidhaa za viwandani, Tafadhali waelekeze wadau wote wa mizani unayo iendesha kuzingatia maelekezo haya ili kuepuka usumbufu kwa wafanya biashara". Amesisitia Hamsin.
Awali akiongea mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt, Ashatu Kijaji, Meneja msaidizi wa kiwanda cha magodoro ya Tanfoam Jijini Arusha Ndg, Meshack alisema halmashauri hiyo imekuwa ikiwalazimisha kwenda mizani ndipo wazunguke kwenye maghara yao kwa lengo la kulipa shilingi elfu 5000 za mizani kama njia ya kuongeza mapato ya ndani ya Jiji hilo kitu ambacho kinachelewesha ufanisi wa utendaji wa kazi na ustawi wa biashara.
![]() |
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt, Ashatu Kijaji akizungumza na waandishi wa habari |
Kufuatia malalamiko kadha wa kadha ya wafanya biashara mbalimbali juu ya mizani hiyo ya ngarenaro Waziri Dkt, Kijaji alimwelekeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela pamoja na Mkurugenzi wa Jiji hilo Juma Hamsin kulitatua kwa haraka ili kuepusha usumbufu kwa wafanya biashara.
![]() |
Taarifa rasmi ya Jiji kusitisha upimaji wa magari ya mizigo inayosambazwa katika Jiji la Arusha |
No comments:
Post a Comment