![]() |
Baadhi ya waandishi wa habari Arusha wakiwa katika kongamano la Arusha tourism Festival la mwaka 2017 |
![]() |
Aliyekuwa afisa Utalii Mkoa wa Arusha Flora Basil alipokuwa akizungmza katika kongamano la Arusha Tourism Festival |
![]() |
Majuto Omary Mwenyekiti wa Taswa Fc ya jijini Dar es Salaam akizungumza katika tamasha la Arusha Tourism Festival |
Mwandishi
wetu, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Tamasha
la nane la Utalii na wanahabari, Arusha tourism Festival linatarajiwa kufanyika Octoba12 hadi 14, 2023 jijini Arusha kwa kuwashirikisha wanahabari na
wadau wa sekta ya Utalii na Uhifadhi nchini.
Tamasha
hilo, linaandaliwa na Taasisi ya Arusha Media kwa kushirikiana na Taasisi ya
wanahabari ya MAIPAC na Chama cha
waandishi wa habari za michezo (TASWA).
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mratibu wa Tamasha hilo, Mussa Juma, alisema
tamasha la mwaka huu,litakuwa na matukio matatu, maonesho ya bidhaa za
Utalii, Kongamano kuhusu sekta ya
Utalii na Uhifadhi na michezo.
“Tunatarajia
kushirikisha watu zaidi 700, wakiwepo wafanyabiashara wa sekta ya Utalii, Wataalam wa utalii na Uhifadhi na waandishi wa habari kutoka mikoa 10 nchini
ambayo imekuwa na changamoto ya migogoro
baina ya wanyamapori na binaadamu”alisema
Juma
alisema Octobar 12-14 kutakuwa na Maonesho, Octoba 13 kongamano la wadau wa
Utalii na Octobar 14 kutakuwa na michezo
ambayo itashirikisha timu za Wanahabari na wadau wa Utalii.
“Tumeanza
maandalizi ya Tamasha hili na mwaka huu, limeboreshwa zaidi tofauti na miaka ya nyuma na tunatarajhia kuwakutanisha
wadau wa sekta ya Utalii na Uhifadhi na
wanahabari ili kuwajengewa uwezo masuala mbali mbali ya Utalii na uhifadhi”alisema
Juma
alisema Katika Tamasha hilo, ambalo tangu mwaka 2015, limekuwa likifanyika kauli mbiu mwaka huu, kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na wananchi
lakini pia kutakuwa na mada ya kadhaa ikiwepo Ulinzi wa maeneo ya mapito ya
wanyamapori, kuzuia biashara haramu ya wanyamapori na nyamapori na umuhimu wa vyombo vya habari kukuza sekta
ya Utalii .
“Tamasha
hili linatarajiwa kusaidia kukuza sekta ya Utalii na Uhifadhi lakini kujenga uelewa mzuri kwa wanahabari juu
ya mafanikio na changamoto za sekta hii lakini pia kwa kuwa tutakuwa katika
maadhimisho ya kumbukumbu tangu kifo cha baba wa Taifa Mwalimu Nyerere tamko
lake juu ya uhifadhi na Wanyamapori la
mwaka 1961 linatajadiliwa ”alisema
Juma
alisema wataalikwa watendaji wa Taasisi za Uhifadhi na Utalii, Shirika la hifadhi za Taifa
(TANAPA) Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori(TAWA) Taasisi ya Utafiti wa
wanyamapori(TAWIRI), Jumuiya za hifadhi za Wanyamapori(WMA) Wakala wa Misitu na
Nyuki (TFS) na Wawekezaji katika sekta ya Utalii.
“Tutaendelea
kutoa taarifa juu ya maandalizi ya tamasha hili la Utalii na tunaomba wadau
mbali mbali kuendelea kujitokeza kuliwezesha na kushiriki”alisema

Awali
Mratibu wa Arusha Media, Andrea Ngobole akizungumzia michezo itakayofanyika Octobar 14, alisema kutakuwa na mchezo wa
soka, mpira wa pete,kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mbio za magunia.
“
Kama mnakumbuka timu ya TASWA Dar es
Salaam ndio walikuwa mabingwa watetezi
katika tamasha la saba katika soka na mpira wa pete tayari wamethibitisha kuja
kutetea ubingwa wao “alisema
Ngobole alisema zawadi za mwaka huu,zitatangazwa
hivi karibuni sambamba na wadhamini wote ambao watakuwa
wamejitokeza.

No comments:
Post a Comment