WAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO YA UKATILI WA JINSIA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 7 August 2023

WAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO YA UKATILI WA JINSIA


UTPC yawafunda waandishi,habari za usawa wa kjinsia





NA: MWANDISHI WETU, MOROGORO


UMOJA wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), umetoa mafunzo kwa waandishi wa habari namna ya kuandika habari za usawa wa kijinsia.


Mafunzo hayo yameanza kutolewa leo Agosti 7,2023 ambayo yatachukua muda wa siku mbili kwa ufadhili wa Shirika la Sweden.


Mkurugenzi Mtendaji wa (UTPC) Kenneth Simbaya, akifungua mafunzo hayo amesema lengo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari, namna ya kuripoti habari za jinsia, pamoja na kuibua mambo ambayo yamefichika ndani ya jamii na kusababisha ukatili wa kijinsia kuendelea.


"Hakuna Maendeleo bila usawa wa kijinsia" amesema Simbaya.


Aidha, amewataka pia waandishi wa habari kujikita katika kuandika habari za jinsia (Specialize), pamoja na kuandika habari kina zaidi na zenye kuleta uwajibikaji, na kubadilisha mitazamo hasi ndani ya jamii juu ya usawa wa kijinsia.


Naye Ofisa Program kutoka UTPC Hilda Kileo, amesema mafunzo hayo pia yamelenga kufanikisha malengo endelevu kwa watanzania wote wanawake na wasichana, kama ilivyoainishwa katika lengo namba 5 la SDGs pamoja na kuhakikisha kuwa mipango ya maendeleo ya Tanzania na SDGs zote 17 zinatekelezwa kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.


Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Sweden Tanzania Nasieku Kisambu, amesema wamefadhili mafunzo hayo wakiamini kwamba vyombo vya habari zinauwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko ndani ya jamii kuhusu masuala mazima ya usawa wa kijinsia, na kuahidi kuendelea kushirikiana na UTPC 'kusapoti'masuala ya jinsia.


Nao baadhi ya waandishi wa habari wamesema mafunzo hayo yamewaongezea uwezo katika kuandika habari za usawa wa kijinsia.
Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Kenneth Simbaya akizungumza kwenye mafunzo hayo.


Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Kenneth Simbaya akizungumza kwenye mafunzo hayo.


Deogratius Temba akitoa mafunzo ya usawa wa kijinsia.


Deogratius Temba akitoa mafunzo ya usawa wa kijinsia


.
Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Sweden nchi Tanzania Nasieku Kisambu, akizungumza kwenye mafunzo hayo.


Ofisa Program kutoka UTPC Hilda Kileo, akizungumza kwenye mafunzo hayo


.
Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Sweden nchi Tanzania Nasieku Kisambu akifuatilia mafunzo hayo ya usawa wa kijinsia


.
Waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo ya usawa wa kijinsia


.
Waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo ya usawa wa kijinsia


















Picha ya pamoja mara baada ya mafunzo


No comments: