Wananchi waalikwa kuadhimisha miaka 62 ya uhuru kilele cha Mlima Kilimanjaro - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 29 August 2023

Wananchi waalikwa kuadhimisha miaka 62 ya uhuru kilele cha Mlima Kilimanjaro

 


Naibu Kamishna wa uhifadhi na maendeleo ya biashara Tanapa Herman Batiho akizungumza na waandishi wa habari 



Na Mwandishi Wetu 


maipacarusha20@gmail.com


Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kushirikiana na kampuni za Utalii, wamezindua mpango wa kupanda mlima Kilimanjaro katika kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika.


 Wamealikwa washiriki wanaopenda kupanda mlima huo, kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi wanatarajiwa kupanda Mlima  kwa gharama nafuu ili kushiriki maadhimisho hayo na kutalii.


Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara TANAPA Herman Batiho akizungumza na  wanahabari  jana alisema Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa na utaratibu wa kuadhimisha sherehe za Uhuru wa Tanganyika tangu ulivyopatikana mwaka 1961 kwa kushirikiana na wadau kadhaa wakiwepo wanahabari.


"Maadhimisho haya yamekuwa yakifanyika kwa kupandisha bendera ya nchi yetu katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Tukio hili limekuwa likihusisha kikundi cha wanajeshi wachache wakishirikiana na askari wa Hifadhi za Taifa Tanzania kwa utaratibu wa kampuni ya utalii ya ZARA ambapo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita maadhimisho haya yalipata sura mpya ya ushiriki wa wananchi na kutambulika kwa jina la “Twenzetu Kileleni” ambapo kwa sasa ni msimu wa tatu"alisema


Kamishna Batiho alisema kupitia hamasa kubwa na mwamko wa watanzania wengi katika kipindi hicho ambapo Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania limeongeza wigo kwa kushirikiana na mawakala wote wa utalii kuratibu kampeni za twenzetu kileleni kwa lengo la kuendelea kuhamasisha utalii wa ndani wakati wa maadhimisho ya Uhuru tarehe 9, Disemba.


 Lengo likiwa  ni kuongeza wigo wa utangazaji wa njia nyingi za kupanda Mlima Kilimanjaro na fursa zaidi kwa watanzania kuchagua kampuni na njia wanazotaka kupanda mlima na sio njia ya Marangu tu kama ilivyozoeleka.


“Kati ya kampuni zote tulizozialika kushiriki katika uratibu wa maadhimisho haya ni kampuni tatu ndio zimejitokeza kushiriki kampeni hii katika msimu huu wa tatu. Kampuni hizo ni ZARA, African Zoom na African Scenic.” 



Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Kamishna msaidizi, Angela Nyaki amewaomba watanzania wote kushiriki kuadhimisha sherehe hizo za uhuru katika kilele kirefu zaidi barani Afrika. 


“Niwakaribishe wananchi wa mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani kuja kushiriki nasi katika sherehe hizi za Uhuru katika Paa la Afrika. Nina imani watanzania wengi wana shauku kubwa ya kushiriki  haya maadhimisho, kwa kulipa kidogo kidogo na kwa wale watanzania wenzetu ambao wamewahi kupanda kwa njia ya marangu nitoe wito sasa tuhamie njia nyingine ili tuuone mlima wetu kwa upande mwingine pia” alisema.


Afisa uhusiano wa kampuni ya Zara tours, Ibrahim Othman amesema gharama za kupanda mlima zimepunguzwa ili kuvutia watu wote



"Kupanda mlima  na kushuka ,pamoja na kupata malazi, chakula na vifaa vya kupanda mlima gharama imepunguzwa na haizidi 1.2 milioni"alisema

Elisimbo Natai mkurugenzi wa kampuni ua African Slenic Safari alisema wanatarajia watanzania wengi kujitokeza.


No comments: