BOT wataka wafanyabiashara Mpaka wa Namanga kuacha biashara haramu ya kubadilisha fedha - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 1 September 2023

BOT wataka wafanyabiashara Mpaka wa Namanga kuacha biashara haramu ya kubadilisha fedha

 

Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi wa BOT, Amri Mbarilaki akizungumza na wafanyabiashara na Maafisa wa Serikali katika Mpaka wa Namanga  Agosti 31,2023



Na: Andrea Ngobole, MAIPAC 

maipacarusha20@gmail.com


Benki Kuu Tanzania (BOT) imewataka Wafanyabiashara wa Mpaka wa Tanzania na Kenya wa Namanga kuacha kufanya biashara haramu ya kubadilisha fedha badala yake wafate taratibu za kuwa na Leseni .


Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi wa BOT, Amri Mbarilaki akizungumza na wafanyabiashara na Maafisa wa Serikali katika Mpaka huo wa Namanga Leo Agosti 31,2023 amewataka kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kufanya biashara halali ya fedha za kigeni.


"Tukiendelea na biashara hii haramu uchumi utaharibika na ukiharibika hasara itakuwa kwetu sote hata kwa ambao wanafanya biashara hii"amesema


Amesema ni muhimu ambao wanataka kufanya biashara ya kubadilisha fedha kufuata sheria na Kanuni ikiwepo kuwa na Leseni ya biashara hiyo.


Meneja Msaidizi wa Usimamizi Taasisi za fedha Maalum BOT Omar Msuya alisema Dunia hivi sasa ipo katika ushindani wa kiuchumi ambao unahitaji akiba ya fedha za kigeni.


"Ingawa Tanzania bado tuna akiba ya Dola tofauti na nchi nyingine za jirani lakini ni muhimu kuzingatia sheria katika kufanya biashara ya fedha za kigeni "amesema



Amesema sheria ipo wazi ambao wanafanya biashara hiyo kuanzisha Kampuni na kuwa la leseni lakini kwa wasio na leseni adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 14 au faini au vyote pamoja.


"Sasa tusifikie huko kwenye kufikishana Mahakamani sote tufate sheria kwani ni rahisi sana kuanzisha maduka ya fedha za kigeni"amesema


Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwepo kwa maduka haya na ndio sababu sheria na kanuni zinaendela kuboreshwa Sasa  tuanzishe maduka na tufate sheria .


"Mkuu wa polisi wilaya ya Longido,Leah Ncheyeki  na Afisa Uhamiaji katika Mpaka huo Bulugu Edward walieleza tatizo la biashara haramu ya fedha za kigeni lipo katika Mpaka huo na kutaka wanaojihusisha kuacha mara moja


Ncheyeki amesema katika Namanga kuna biashara kubwa ya kubadilisha fedha kinyume cha sheria lakini pia kuna wanaotoa  fedha bandia kwani elimu ya BOT Sasa ilete mabadiliko kabla ya hatua za kisheria kuanza kuchukuliwa.


 Nkanga hata hivyo amesema Mpaka huo kuna upungufu  wa maduka ya kubadilisha fedha licha ya kupokea watalii ambao wamekuwa na mahitaji ya kubadilisha fedha.


Baadhi ya wafanyabiashara John Kessy alieleza elimu ambayo imetolewa na BOT itasaidia kwani walikuwa na hofu ya kufungua maduka .


"Kutokana na yaliyotokea miaka ya nyuma kunyang'anywa fedha  tulikuwa na hofu Sasa BOT imeondoka hofu ya kuanzisha maduka kwa kuzingatia sheria"amesema.


Biashara haramu ya fedha za kigeni imeelezwa kuchangia kupunguza fedha hizo katika mzunguko kutokana na watu wachache kumiliki fedha nyingi na wengine kusafirisha nje ya nchi kinyume cha sheria. 


No comments: