Macklion na Macedonia zatinga fainali chemchem CUP 2023 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 26 October 2023

Macklion na Macedonia zatinga fainali chemchem CUP 2023

 





Mwandishi wetu, Babati


maipacarusha20@gmail.com


Timu za soka za Macklion na Macedonia zimetinga tena fainali ya michuano ChemChem Cup 2023 ambayo inatarajiwa kuchezwa October 29 katika uwanja wa Mdori wilayani Babati mkoa Arusha.



Michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na Taasisi ya chemchem association kwa zaidi ya sh 100 milioni , inalenga kupiga vita ujangili wa Twiga na mwaka huu timu 31 zimeshiriki.


Macklion ambao ni mabingwa watetezi wa chemchem CUP imetinga fainali kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifunga kwa penati Timu ya Olasiti.


Kwa Upande wa timu ya Macedonia imetinga fainali pia kwa kuiondoa timu ya majengo kwa changamoto ya penati pia baada ya kutoka Suluhu kwa dakika 90.


Kwa Upande wa timu za vijana timu ya Olasiti imetinga fainali baada ya juzi kuichapa timu ya Macklion goli 1-0 na itachuana na Manyara FC ambayo nayo iliitoa timu ya Macedonia kwa kuichapa 1-0.


Katibu wa michuano ya chem chem CUP, John Bura alisena timu ya wanawake ya Mwada itachuana na timu ya Maweni.


"Maandalizi ya michezo ya fainali na mshindi wa tatu yanaendelea na mgeni Rasmi atatangazwa"alisema


Katika michuano ya mwaka huu ambayo ilifunguliwa na Mkuu wa mkoa Manyara, Queen Sendiga ambapo mkurugenzi wa chemchem  association Fabia Bausch alisema michuano hiyo tangu imeanzishwa imekuwa na faida kubwa kushirikisha jamii katika uhifadhi kupitia uhifadhi.


Fabia alisema mwaka huu  kwa mara ya kwanza kumekuwa na timu 10 za wasichana za mchezo wa soka, timu 16 za wanaume na timu 7 za vijana.


Amesema taasisi hiyo imetenga kutimia zaidi ya sh 100 million kufanikisha michuano ya mwaka huu.


Bingwa wa soka wakubwa atapewa zawadi ya sh 2.5 milioni, wa pili 1.5 milioni na wa tatu 1 milioni. Kwa upande wa wasichana mabingwa watapata 1.5 milioni, mshindi wa pili million Moja na mshindi wa tatu 500,000.


Kwa michezo kwa vijana chini ya miaka 18 mshindi atapata milioni Moja wa pili 600,000 na wa tatu 400,000 ambapo timu zote zimepewa seti ya jezi na mipira.



No comments: