MWENYEKITI WA CCM MKOA WA ARUSHA, ZELOTHE STEVEN AFARIKI DUNIA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 26 October 2023

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA ARUSHA, ZELOTHE STEVEN AFARIKI DUNIA



 
ZELOTHE STEVEN enzi za uhai wake



Na Mwandishi Wetu, Maipac 


maipacarusha20@gmail.com


Aliyekuwa Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Arusha ZELOTHE STEVEN Amefariki dunia jioni ya Leo October 26 jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.


Kwa mujibu wa taarifa za kifo chake zilizothibitishwa pia na katibu wake Musa Matoroka, zinasema mwenyekiti huyo amefariki akiwa anapatiwa matibabu jijini Dar es Salaam na msiba upo nyumbani kwake sea view Upanga jijini Dar es Salaam na taarifa zaidi za mazishi zinatarajia kufanyika kwa siku itakayopangwa nyumbani kwake Olasiti jijini Arusha.

ZELOTHE STEVEN akiwa mtumishi wa jeshi la polisi


ZELOTHE STEVEN Akiwa mtumishi wa jeshi la polisi aliwahi kuwa Kamanda wa polisi katika Mikoa ya Arusha , Dodoma, Mwanza na Mbeya ambapo alidhibiti sana uhalifu katika Mikoa hiyo.

Chanzo cha kifo imeelezwa kuwa ni maradhi yaliyokuwa yakimsibu kwa muda mrefu na kumfanya kupotea kwa muda kwenye duru za kisiasa na kutumia muda huo kupata matibabu.



No comments: