MAKONDA ATEULIWA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 22 October 2023

MAKONDA ATEULIWA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA

 

Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa itikadi na Uenezi CCM Taifa


Na Andrea Ngobole, Arusha 


maipacarusha20@gmail.com


Aliyewahi kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Leo Jumapili October 22 ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi.


Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo Habari  na umma iliyotolewa na sekretariet ya Chama Imesema kuwa Kikao maalumu cha Kamati kuu ya Chama kwa kauli Moja imeazimia kumteua Paul Makonda kuwa Katibu Itikadi na Uenezi ya Chama akichukua nafasi ya Sofia Mjema aliyeteuliwa  Kuwa mshauri wa RAIS wa masuala ya wanawake na makundi maalumu.


Makonda ambaye aligombea kura za maoni ndani ya CCM kuteuliwa kugombea ubunge  Jimbo la Kigamboni Daresalaam na kushindwa na Dkt Ndugulile ambaye ndiye mbunge wa Kigamboni kwa sasa, Amekuwa kimya katika mambo ya uongozi wa Chama na Serikali kwa takribani miaka mitatu sasa.


 KATIKA taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ya Kamati kuu pia imeridhia Serikali kuingia Mkataba  wa Bandari ya Dar es Salaam na kampuni ya DP world ili kuendeleza malengo ya ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.



No comments: