NAIBU WAZIRI KIGAHE APONGEZA UWEKEZAJI WA KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS LTD - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 19 October 2023

NAIBU WAZIRI KIGAHE APONGEZA UWEKEZAJI WA KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS LTD

 



Na Mwandishi wetu, Babati 

 

maipacarusha20@gmail.com


NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe ameipongeza Kampuni ya Mati Super Brands ambao ni wazalishaji wa vinywaji vikali kwa uwekezaji wa viwanda walioufanya na kushiriki kudhamini maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair yanayoendelea katika viwanja vya Stendi ya zamani ya Mjini Babati Mkoani Manyara.

 

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la kampuni ya Mati Super Brands Limited Naibu Waziri Kigahe amepongeza juhudi za kampuni hiyo katika kuwekeza na kulipa kodi stahiki ya Serikali.

 

Kigahe amesema kampuni hiyo imekua mstari wa mbele katika kutoa misaada kwa jamii inayowazunguka pamoja na kudhamini matukio mbali mbali ya kijamii na kiserikali.

 

Hata hivyo, Meneja Masoko wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited Elvis Peter amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora wa kitaifa na kimataifa.

 

“Kampuni yetu imekua ni wadhamini wakuu wa Maonyesho ya Tanzanite Manyara TRADE FAIR ambayo yanakutanisha wafanyabishara kutoka ndani na nje ya nchi,” Ameeleza Elvis.


Mmoja kati ya wajasiriamali walishiriki maonyesho hayo, Elias Baha amesema wawekezaji wengi zaidi waende kuwekeza kwenye mkoa huo ili jamii ipate ajira kama ilivyofanya kampuni ya Mati Super Brands LTD.


"Wawekezaji wengi zaidi tunawataka mje kuwekeza Manyara mfanye mambo mengi kama ilivyo Mati ni pana ndiyo sababu tunawapongeza kwa uwekezaji wao," amesema Baha.




No comments: