WANAFUNZI WA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII (NCT) KUFANYA MAZOEZI YA UTENDAJI KAZI NCHI ZA ULAYA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 19 October 2023

WANAFUNZI WA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII (NCT) KUFANYA MAZOEZI YA UTENDAJI KAZI NCHI ZA ULAYA

 



Na: Mwandishi wetu-Dar es salaam


maipacarusha20@gmail.com


Wanafunzi wa chuo cha Taifa cha  Utalii nchini Tanzania (NCT) wanatarajiwa kuanza kufanya mazoezi ya utendaji kazi  katika nchi za Denmark, Norway, Ujerumani na Sweden.


Haya yamebainishwa na Mkuu wa Chuo hicho,  Dkt. Florian Mtey baada ya kutembelewa na Mkurugenzi  Mkuu wa kampuni ya Bixter.work,  Bi. Nataliya Jorgensen na Mkuu wa Kituo cha SUGECO  Bw. Revocatus Kimario ofisini kwake jijini Dar es salaam.


Dkt. Mtey amebainisha kwamba fursa hii ambayo wanafunzi wa chuo hicho cha  Utalii wanaenda kuipata italeta tija katika fani ya ukarimu kwa vile kwa sasa soko la utalii nchini limekuwa kubwa  kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya kutangaza utalii ya The Tanzania Royal Tour.


Awali, wakitembelea chuo hicho katika Kampasi ya Dar es Salaam, Bi. Nataliya kutoka Bixter.work na Bw. Kimario kutoka SUGECO kwa pamoja  wamefurahi sana kuona Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)  kinatumia  vifaa bora na vya kisasa kutoa mafunzo ya Ukarimu na upishi, na kwamba kwao itakuwa ni fursa kubwa kwa kuchangia mafunzo ya  wataalamu wa ukarimu katika nchi ya Tanzania.




No comments: