Tume ya Afrika ya Haki za Binaadamu na Watu yashauri Mazungumzo Ngorongoro, yabaini mambo manne. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 26 October 2023

Tume ya Afrika ya Haki za Binaadamu na Watu yashauri Mazungumzo Ngorongoro, yabaini mambo manne.

 





John Lukumay ,Maipac

maipacarusha20@gmail.com


Tume ya Afrika ya Haki za Binaadamu na Watu (ACHPR) imetoa taarifa ya awali juu ya ziara yake ya nchini, kufatilia mgogoro wa Ngorongoro na kueleza kuna haja ya kuwepo mazungumzo baina ya pande zote ili kumaliza mgogoro.


Tume hiyo imeeleza kubaini mambo manne katika ziara ya Makamishna wa Tume hiyo waliotembelea wilaya ya Ngorongoro mkoa Arusha na Msomera mkoani Tanga ambayo yatafafanuliwa kwenye ripoti ambayo itatolewa Karibuni.


Hayo yanebainika katika kikao kilichoandaliwa na Taasisi za kimataifa za Amnesty international, Protection international Afrika,Minority Rights group international na Human Rights Watch ikiwa na sehemu ya Vikao vya pembeni vinavyoendana na Kikao cha 77 Cha ACHPR kinachoendelea hapa jijini Arusha.


Akizungumza kwenye kikao hicho Kamishna wa Tume hiyo ambaye anashughukikia Jamii za pembezoni Dkt. Litha Ogana alisema ingawa taarifa rasmi ya tume itatolewa karibuni ila Kuna mambo manne ambayo waliyaona.


Dkt. Ogana alisema mambo waliyobaini kwa Ngorongoro kuna Jamii ya watu wanataka kuhama kwa hiari na wengine hawataki na kwa Loliondo kulikuwa na changamoto ya ushirikishwaji Jamii na matumizi ya nguvu kutenga eneo la hifadhi.


Alisema Tume inakamilisha taarifa yake na itakabidhiwa serikali ya Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya utekelezwaji wa mapendekezo yao kwani tayari iliwasilisha vielelezo vyake kwa tume hiyo.


Hata hivyo alisema baada ya taarifa hiyo kukabidhiwa serikalini, serikali ndio itakuwa na wajibu wa kutekeleza mapendekezo ya tume au la kwa ushirikiano na wananchi.


Dkt. Ogana hata hivyo alisema mgogoro wa Ngorongoro na Loliondo hautamalizwa na taarifa ya tume Bali kwa Kukaa pamoja  Jamii kupitia viongozi wao na serikali .


" Wananchi wa Ngorongoro, Loliondo na Msemora wanapaswa kuwa watulivu wakati tume inaendelea kukamilisha kuandika taarifa yake rasmi"alisema 


Awali wakizungumza katika kikao hicho, Wakili Joseph Ole Shangay, Wakili Edward Porokwa na Mtafiti wa Shirika la Amnesty international Roland Ebole walieleza changamoto kadhaa za Jamii za pembezoni na kukosekana Uhuru wa kujieleza.


Wakili Oleshangay alisema, wamefanya jitihada kadhaa kutatua migogoro ya Ngorongoro na Loliondo ikiwepo kufikisha Mahakamani mashauri kadhaa lakini bado Suluhu haijapatikana.


Wakili Porokwa ambaye ni mkurugenzi wa Shirika la PINGOs Forums alisema hofu imetawala Ngorongoro na kusababisha Asasi za kiraia hata vyombo  vya habari vya ndani kushindwa kufanya kazi.


"Hata kuzungumza hapa watu wanahofu hawajuwi hali itakuwaje hivyo Uhuru wa kujieleza umepungua sana kutokana na mgogoro huu"amesema


Baadhi ya wananchi wa Ngorongoro, Loliondo, Msomera, Mara na Malinyi na wawakilishi wa Asasi za kiraia ndani na nje ya nchi wakizungumza katika kikao hicho, waliomba tume isaidie kumaliza mgogoro katika wilaya ya Ngorongoro, Msomera na maeneo mengine ya Jamii za pembezoni Afrika.


Wazungumzaji wa Asasi za kiraia wa Kenya na Rwanda walieleza Shida za Jamii za pembezoni kufanana katika nchi kuchukuliwa ardhi na wakaomba tume ya Haki za Binaadamu na Watu Afrika kusaidia.


No comments: