WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI ARUSHA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 26 October 2023

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI ARUSHA




Na Mwandishi Wetu, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) amewasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K.Mongella na viongozi wengine wa Chama na Serikali pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Arusha, kwenye Uwanja wa Ndege Arusha kwa Ndege ya Air Tanzania.


Mhe. Waziri Mkuu yuko mkoani Arusha kwa ajili ya kufungua mkutano mkuu wa 9 wa Wadau wa Lishe, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha 26.10.2023.


Mkutano wa 9 wa Wadau wa Lishe 2023 umebeba Kauli mbiu ya "Kuimarisha Mifumo Endelevu ya Chakula kwa Maendeleo Bora ya Lishe na Maendeleo ya Rasilimali Watu"




No comments: