Watatu wafa ajalini Vigwaza - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 24 October 2023

Watatu wafa ajalini Vigwaza

 



NA MWANDISHI WETU , MAIPAC KIBAHA


WATU watatu wamefariki dunia katika ajali ya barabarani iiliyohusisha magari mawili kugongana uso kwa uso katika Kijiji cha Mbala, Kata ya Vigwaza Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Tukio la ajali hiyo lilitokea saa tatu usiku wa kuamkia Octoba 24 ambapo gari dogo aina ya Kluger yenye namba za usajili T.478 DCQ ikitokea Iringa kwenda Dar es Salam likiwa na watu 7 wa familia moja iligongana na gari lenye namba T.851 AQC aina ya Scania iliyokuwa ikitokea Dar es Salam kwenda Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema katika ajali hiyo watu wanne walijeruhiwa akiwemo Amina Kondo (77), Abdallah Ally (1) wakazi wa Manzese jijini Dar Es Salam pamoja na wanaume wengine wawili ambao hawajafahamika majina yao.

Kamanda Lutumo amesema majeruhi na waliofariki wote walitoka kwenye gari ndogo iliyokuwa ikitokea Iringa kwenda Dar es Salam ambayo ilikuwa imepakia ndugu wa familia moja.

Ameeleza kwamba chanzo cha ajali hiyo ni gari ndogo kutaka kuiyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari na hivyo kugongana uso kwa uso na Lori hilo ambalo lilijaribu kukwepa gari ndogo bila mafanikio.

No comments: