Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha, Blandina Nkini, akizungumza katika mafunzo maalumu ya jukwaa la mwanamke kijijini KATIKA kata ya kimnyaki mapema leo |
Na Prisca Libaga Arusha
maipacarusha20@gmail.com
WAZIRI wa maendeleo ya Jamii Jinsia na makundi maalumu, Dkt Dorothy Gwajima, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini ,duniani itakayoadhimishwa Kijiji cha Olevolos kata ya Kimnyaki, Wilayani Arumeru Mkoani Arusha kesho Oktoba 15.
Madhimisho hayo kitaifa yanafanyika Kijijini hapo kutokana na Kijiji hicho kuanzisha Sheria ya kutoa adhabu kwa Kila mkazi atakae kiuka maadili ikiwemo kuvaa mavazi ya mlegezo maalumu kata K na kunyoa kiduku watatozwa shilingi elfu 50.
Lengo la kuanzishwa Sheria hiyo ni kudumisha maadili yaliyo mema na kuweza kuwarejesha wale wote walioacha maadili kurejea kwenye maadili mema ambayo yatakuwa ni mfano wa kuigwa.
Akifungua mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Jukwaa la Mwanawake Kijijini 2023 kwenye uwanja wa Kijiji cha Olevolosi kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha, Blandina Nkini, amehimiza Jamii kuzingatia maadili Ili kuondoa mmomonyoko wa maadili ambao kwa sasa limekuwa ni tishio kubwa kwa wananchi wa Vijijini na mijini.
Amesema chanzo cha mmomonyoko wa maadili ni familia kuyumba na kushindwa kutimiza majukumu na uwajibikaji kunakosababisha mmomonyoko wa maadili hivyo iwapo familia zitasimama imara mmomonyoko huo hautakuwepo.
Amesema kuwa Wanawake ndio wazalishaji wakubwa lakini wamekuwa wakikandamizwa Kwa kunyimwa haki ya kumiliki mali na kushirikishwa kwenye maamuzi.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Arusha, Denis Mgie, amesema kuwa Kijiji hicho kimeweka Sheria hiyo baada ya kuwepo changamoto Katika malezi, hivyo Kijiji hicho kimekuwa Wakala mkubwa wa mabadiliko katika malezi na makuzi ya watoto nchini.
Amesema kuwa kauli ya kusema sitaki mtoto wangu ateseke imetumika vibaya tulizania tumelea kumbe tumeharibu.
Amesema kuwa Jamii inatakiwa kuongoza Kwa misingi mizuri kwa kuweka misingi ya watoto na Vijana Ili kuelewa nafasi ya mzazi au mlezi .
Amesema mmomonyoko wa maadili pia unaochangiwa na baadhi ya wazazi au walezi kutokuwajibika kulea watoto kwa kuacha jukumu hilo la kulea watoto kwa dada wa kazi na matokeo yake mtoto akiwa mkubwa atampeleka mzazi kwenye Kituo cha kulea wazee
Amesisitiza kwamba malezi ya watoto ni nguzo muhimu Katika kuelekea kuwa na taifa lenye watu wanaojitambua.
Kauli mbiu ya madhimisho hayo inasema Wezesha Wanawake wanaoishi Kijijini kwa uhakika wa chakula , lishe na uendelevu kwa familia .
No comments:
Post a Comment