WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA TARURA KWA KAZI WANAYOIFANYA, AFURAHISHWA NA TEKNOLOJIA MBADALA YA UJENZI WA BARABARA NA MADARAJA YA MAWE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 27 October 2023

WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA TARURA KWA KAZI WANAYOIFANYA, AFURAHISHWA NA TEKNOLOJIA MBADALA YA UJENZI WA BARABARA NA MADARAJA YA MAWE

Waziri  wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Mohammed Mchengerwa, akizungumza  na watumishi wa TARURA  katika kikao cha watumishi wa Wakala huo kilichofanyika  Makao Makuu ya TARURA jijini Dodoma




Na. Catherine Sungura,Dodoma


maipacarusha20@gmail.com


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kazi kubwa wanayofanya tangu kuanzishwa kwakwe.


Waziri Mchengerwa ameyasema hayo jana wakati wa kikao chake na Menejimenti na watumishi wa TARURA kilichofanyika ofisi za TARURA zilizopo mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.


Mhe. Mchengerwa amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Wakala huyo mwaka 2017 kumekuwa na ongezeko la barabara Za lami kutoka kilomita 1,449.55 hadi kilomita 3,053.26 sawa na ongezeko la  110% pia barabara za changarawe zimeongezeka kutoka kilomita 24,405.40 hadi kilomita 38,141.21 sawa na ongezeko lako la 56%.


“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeongeza fedha za matengenezo,ukarabati na ujenzi wa barabara na madaraja kutoka Bilioni 275.03 mwaka 2020/21 hadi kufikia Bilioni 836.237 kWa mwaka wa fedha 2021/22,2022/23 sawa na ongezeko la 204% na mwaka huu 2023/2024”.Amesema Mhe. Mchengerwa.


Aidha, ameipongeza TARURA kwa kutumia teknolojia mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ya mawe (cobble stone roads) na madaraja ya mawe (stone arch bridges) na majaribio ya teknolojia nyingine katika kuboresha barabara wanazosimamia.


Hata hivyo ameitaka TARURA  kulipa kipaumbele jukumu la  kukuza na kuwaendeleza wakandarasi wazawa ili kutoa mchango mkubwa kwa Taifa na kuwataka kuwatambua makampuni ya wakandarasi ishirini kila mkoa.


Naye,Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amesema wataendelea kufanya kazi ili kutimiza malengo ya TARURA na kuhusu kukuza wakandarasi wazawa amesema watashirikiana na bodi ya wakandarasi nchini pamoja na taasisi za kifedha.


Matumizi ya teknolojia mbadala Mhandisi Seff amesema teknolojia hiyo ndio muelekeo wa TARURA wa kupunguza gharama na kutunza mazingira.






Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Rogatus Mativila akiongea na watumishi wa TARURA(hawapo pichani) wakati wa kikao cha pamoja na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohammed Mchengerwa



No comments: