RAIS WA SUDAN MHE. SALVA KIIR MAYARDIT AWA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 24 November 2023

RAIS WA SUDAN MHE. SALVA KIIR MAYARDIT AWA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

 



Na Elinipa Lupembe


Rais wa Sudan Mhe. Salva Kiir  Mayardit, amekuwa Mwenyekiti wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baaaya kupokea kijiti kutoka kwa Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye, ambaye  amemalliza muda wake.


Mara baada ya kuchaguliwa, Mhe. Salva Kiiri, amekabidhiwa nyenzo za kufanyia kazi, kwa kipindi chote cha kuiongoza Jumuiya hiyo, nafasi ambayo inadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.


Hata hivyo Marais wa Jumuiya hiyo, kwa pamoja, wamempongeza kwa kuchaguliwa na kumtakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu yake, huku wakimsisitiza kuendeleza na kuimarisha mtangamano muhimu wa nchi hizo, kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.


Awali, Mkutano wa 23 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki, umefanyika kwa siku mbili mkoani Arusha,  ukitanguliwa na vikao vya ndani na umemalizika jioni ya leo tarehe 24 Novemba, 2023, Ngurdoto wilayani Arumeru.


#eastafricacommunity

No comments: