RC MONGELLA ASHIRIKI HAFLA YA UZINDUZI WA OFISI YA UBALOZI MDOGO WA UGANDA MKOA WA ARUSHA. πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΊπŸ‡¬ - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 25 November 2023

RC MONGELLA ASHIRIKI HAFLA YA UZINDUZI WA OFISI YA UBALOZI MDOGO WA UGANDA MKOA WA ARUSHA. πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΊπŸ‡¬

 




Na Elinipa Lupembe, Arusha


maipacarusha20@gmail.com



Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K.Mongella ameshiriki hafla ya uzinduzi wa Ubalozi Mdogo wa Uganda mkoani Arusha, eneo Uzunguni barabara ya  Haile Sellasie, Jijini Arusha.


Akizungumza kwenye halfa hiyo, Mhe. Mongella ameishukuru Serikali ya Uganda, kwa kufungua ofisi ndogo za Ubalozi mkoani humo, kutokana na umuhimu wake wa uhusiano wa miaka mingi kati ya watu wa Arusha na watu wa Uganda na kukiri kuwa, Ofisi hizo zimechelewa kufunguliwa mkoani hapo.


Amethibitisha kuwa, upo uhusiano mkubwa na uliodumu kwa miongo mingi kati ya Tanzania na Uganda, hasa kwa kuzingatia Uganda ni miongoni mwa nchi za kwanza, kuungana na kuunda Jumuia ya Nchi za Afrika Mashariki na kuahidi kutoa ushirikiano wa kiseta wakati wote kama yalivyo maelekezo ya Serikali ya awamu ya sita.


"Serikali ya Tanzania, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetuelekeza kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kwa nchi yoyote itakayofungua ofisi ndogo za balozi mkoani hapa, niwaahidi kudumisha ushirikiano baina yetu, zaidi niwakaribishe Arusha, ninaamini mtafurahia kuwepo Arusha" Ameweka wazi Mhe. Mongella.


Ofisi ndogo za Ubalozi wa Uganda mkoani Arusha zipo, Barabara ya Haile Selassie na 20B, Jiji la Arusha.








No comments: