Rufaa ya Lengai Ole Sabaya Yasikilizwa, Mawakili wake wasisitiza hana hatia - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 1 November 2023

Rufaa ya Lengai Ole Sabaya Yasikilizwa, Mawakili wake wasisitiza hana hatia



Lengai Ole Sabaya akizungumza na mawakili wake katika chumba Cha Mahakama ya rufaa mapema leo


 Na Mwandishi Wetu Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Kesi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya kukatiwa rufaa na jamhuri  imesikilizwa leo katika mahakama kuu kanda ya Arusha huku upande wa serikali wakieleza hoja zao saba  mbele ya  majaji watatu wa rufani.


Kesi  hiyo yenyevuto wa kipeke imesikilizwa kwa muda wa masaa saba ambapo pia mabishano ya kisheria kwa upande wa utetezi wa sabaya na serikali ulikua mkubwa ambapo majira ya saa kumi na moja jioni kesi hiyo ilimalizika na huku majaji wakisema maamuzi ya rufani hiyo itatolewa baadae kupitia kwa msajili wa mahakama kutoa taarifa kwa mawakili wa pande zote mbili.


Kesi ilikua ikisikilizwa na majaji watatu wakiongozwa na Mwenyekiti Jaji Jacobs Mwambegele, Jaji Ignas Kitusi na Jaji Leila Mgonya

 

Mawakili watetezi wa Sabaya wakiongozwa na WAKILI  Msomi Mahuna na Sylvester Kahunduka wamesisitiza mteja wao hana hatua


No comments: