Wadau wa habari na Asasi za kiraia wajadili usawa wa kijinsia na Uhuru wa habari - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 25 November 2023

Wadau wa habari na Asasi za kiraia wajadili usawa wa kijinsia na Uhuru wa habari

 

Wadau wa habari wakijadiliana namna Bora ya kupinga ukatili wa jinsia na kikuza uhuru wa vyombo vya habari 
 

Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Wafanyakazi katika vyombo vya habari nchini (JOWUTA),Mussa Juma amesema wao wanataka sera ya jinsia katika vyombo vya habari na maslahi Bora kwa waandishi wa habari 

Mkurugenzi wa MISA TAN , Elizabeth Riziki akizungumza katika siku ya kupinga ukatili wa jinsia


Gladness Munuo Mratibu wa Shirika la wanahabari la utetezi masuala ya jinsia ( GEMSAT) akizungumza na wadau wa habari katika siku ya kupinga ukatili wa jinsia 


MISA Tan yataka ushirikiano kutokomeza ukatili


JOWUTA yataka sera ya jinsia katika vyombo vya habari na Maslahi bora



Mwandishi wetu,Dar es Salaam


maipacarusha20@gmail.com


Wadau wa habari nchini,wametaka kuwepo Jukwaa la pamoja ambalo litashirikisha Taasisi za wanahabari, Asasi za kiraia Serikali na Mshirika la Umoja wa Mataifa katika kutokomeza ukatili wa kijinsia na kukuza Uhuru wa habari nchini.


Wakizungumza katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili  wa kijinsia yaliyofanyika ukumbi wa Umoja wa Mataifa jijini Dar es salaam(UNIC) wadau hao wa habari,Serikali na asasi za kiraia walieleza lazima hatua zichukuliwe kukomesha ukatili.


Walieleza kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA TAN) kwa kushirikiana na  Shirika la kimataifa la VIKES ni muhimu kwani licha jitihada kadhaa kufanyika lakini bado kuna changamoto ya matukio ya Ukatili lakini kiminywa kwa Uhuru wa Vyombo vya habari.


Mkurugenzi wa MISA TAN , Elizabeth Riziki amesema ni muhimu kuimarisha ushirikiano, kubadilishana mawazo, na kuwa na mikakati itakayochangia kukuza usawa wa kijinsia na uhuru wa vyombo vya habari.



“MISA tunataka kuunda jukwaa ambalo litahusisha serikali, wataalamu wa vyombo vya habari, na wawakilishi wa taasisi za kijamii kujenga uhusiano, mikakati ya pamoja  ili kukomesha matukio ya ukatili"amesema na kuongeza 


“Lengo jingine ni Kujiandaa kwa Siku 16 za Uanaharakati kwa kuunganisha nguvu katika kampeni kubwa ya kimataifa ya Siku 16 za Uanaharakati Dhidi ya Dhuluma za Kijinsia, kuunda msukumo kwa juhudi endelevu zaidi baada ya tukio la siku moja”,ameeleza.


Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Wafanyakazi katika vyombo vya habari nchini (JOWUTA),Mussa Juma akitoa mada katika kongamano hilo,amesema ni muhimu vyombo vya habari kuwa na sera ya jinsia na madawati ya Jinsia.


Amesema katika vyombo vya habari Kuna matukio ya Ukatili wa kijinsia ambapo waathirika wakubwa wamekuwa ni Wanawake lakini wanakosa sehemu sahihi za kufikisha malalamiko lakini pia hakuna mikakati ya kukomesha matukio ya Ukatili.


"Kukosekana kwa sera za Jinsia ,Maslahi duni ya wanahabari na imekuwa ni miongoni mwa changamoto ambazo zinachangia ukatili wa kijinsia"amesema


Amesema wanahabari nchini zaidi ya asilimia 80 hawana ajira Wala mikataba ya Kazi jambo ambalo linachangia kuongezeka matukio ya kufanyiwa ukatili.


Hata hivyo amesema wanahabari nchini kujiunga na vyama vya wafanyakazi ili pia iwe rahisi kufatilia changamoto zao kisheria na hatua kuchukukuliwa.


Mkurugenzi mstaafu wa MISA-Tan na mwanahabari Mkongwe nchini,Rose Haji Mwalimu amesema Kuna jitihada kubwa ziliwahi kufanywa na Asasi kadhaa ikiwepo Chama chama Cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA),kuelimisha kuundwa sera ya jinsia la baadhi ya vyombo vikaunda lakini hakuna utekelezwaji.


"Tulitoa elimu kubwa kwa vyombo vya habari na hadi katika radio za kijamii walieleza kuwa na sera za jinsia lakini naona hazifanyiwi kazi ama kuboreshwa"amesema.


Katibu Mtendaji wa Baraza la watumiaji wa huduma za Mawasiliano(TCRACCC),Mary Msuya amesema Baraza limekuwa likipokea malalamiko ya ukatili katika mitandao na Wanawake wanaongoza kufanyiwa ukatili.


"Ukatili katika mitandao ni mkubwa na tunaendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ili kukomesha Ukatili"amesema


Gladness Munuo Mratibu wa Shirika la wanahabari la utetezi masuala ya jinsia ( GEMSAT)  akitoa mada katika kongamano hilo amesema ni muhimu kuwepo ushirikiano wa pamoja kukomesha ukatili katika vyombo vya habari na Uhuru wa Vyombo vya habari.


Amesema GEMSAT katika tafiti zake bado wamebaini kuendelea ya ukatili dhidi ya wanawake katika nyanja za kiuchumi kisiasa na maeneo mengine lakini Asasi za kiraia zinapaswa kuwa na mikakati ya kuwashirikisha pia wanahabari katika mafunzo ya Jinsia,ujasiriali na mengine kwani wamekuwa nyuma.


"Ni kweli suala la maslahi ya wanahabari ni muhimu sana kufanyiwa kazi kwa sababu linachangia pia ukatili lakini pia sisi kama Asasi tutenge bajeti kusaidia wanahabari mafunzo na kuboresha Utendaji lakini tujuwe jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi "amesema


Wakili James Marenga amesema matukio mengi ya ukatili hayafikishwi Mahakamani na yake yanayofikishwa kumekuwepo na changamoto ikiwepo waathirika kutaka kumaliza nje ya Mahakama ama kutotokea Mahakamani.


"Kuna kesi kadhaa wasichana wamefanyiwa ukatili lakini zinaishia katikati na hii ni changamoto lakini sisi kama mawakili tupo tayari kusaidia kesi za kupinga ukatili na kutoa elimu ya Uhuru wa Vyombo vya habari "amesema


Afisa habari wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN Tanzania) Didi Nafisa amesema Mashirika ya Umoja wa Mataifa yapo tayari kuendelea kushirikiana na Taasisi za wanahabari na Asasi za kiraia katika kukomesha ukatili wa kijinsia na kuendeleza Uhuru wa habari.


"Tutaendelea kushirikiana kuhakikisha changamoto za masuala ya ukatili zinapatiwa ufumbuzi lakini pia kutetea Uhuru wa Vyombo vya habari"amesema.


No comments: