DKT. YONAZI AISHUKURU REDCROSS KWA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAAFA HANANG’ - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 9 December 2023

DKT. YONAZI AISHUKURU REDCROSS KWA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAAFA HANANG’

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Tanzania Red Cross Bw. Reginald Mhango alipowatembelea na kuzungumza nao katika Shule ya Katesh A ambapo wameweka kambi kwa lengo la kuendelea kutoa huduma kwa waathirika wa Maafa ya Maporomoko ya mawe na Tope Hanang’ Manyara.

 


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akisaini kitabu cha wageni alipowatembelea watumishi wa Tanzania Red Cross Society waliopo Hanang’ kutoa huduma kwa waathirika wa Maafa ya Maporomoko ya mawe na Tope wilayani humo.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akipokea zawadi ya kofia kutoka kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Tanzania Red Cross Society Bw. Reginald Mhango alipowatembelea


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (mwenye kofia nyekundu katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Tanzania Red Cross Society

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)



NA: MWANDISHI WETU, MANYARA


maipacarusha20@gmail.com


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameushukuru uongozi wa Taasisi ya Tanzania Red Cross Society kwa namna wanavyoendelea kujitolea na kutoa misaada mbalimbali kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope na mawe yaliyotokea Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara.


Ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na watendaji wa Red Cross walioweka kambi katika Shule ya Katesh A kwa lengo la kuendelea kutoa huduma kama ilivyohitajika kwa kuzingatia kanuni na taratibu zao.


Dkt. Yonazi amesema Serikali inatambua na kujali mchango wao kwa namna walivyojitoa katika kusaidia waathirika wa tukio hilo huku akitoa rai kwa wadau wengine kuendelea kuunga mkono jitihada hizo katika kuwahudumia mahitaji waliyonayo.


Aliongezea kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi hao wanakuwa katika mazingira mazuri na kuendelea na shughuli zao za uzalishaji kwa utulivu kama ilivyokuwa awali.


“Red Cross mmeendelea kuwa sehemu ya zoezi hili kubwa la kusaidia na kurejesha hali za ndugu zetu huku Hanang’ kwa niaba ya Serikali yetu tunawashukuru sana kwa michango yenu ya hali na mali mliotoa, asanteni sana,” alisisitiza Dkt. Yonazi


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Tanzania Red Cross Society Bw. Reginald Mhango amesema kuwa wataendelea kuungana na Serikali katika kila hatua kuona namna wanavyorejesha hali na kusaidia jamii ya wana Hanang’ waliofikwa na maafa hayo.

No comments: