Halmashauri jiji la Arusha washirikiana na Barick Gold Kujenga shule ya Mchepuo wa Sayansi Kwa wasichana - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 20 December 2023

Halmashauri jiji la Arusha washirikiana na Barick Gold Kujenga shule ya Mchepuo wa Sayansi Kwa wasichana





Na: Andrea Ngobole, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Barrick Gold Mine imetoa kiasi cha  Shilingi 670.1 Milioni zilizowezesha kukamilisha ujenzi wa madarasa 15 na mabweni mawili ya shule ya sekondari ya wasichana Arusha (Arusha Girls High school.)

 KATIKA kukamilisha madawati, vitanda na samani za ofisi za shule hiyo Halmashauri  ya jiji la Arusha limetoa zaidi ya shilingi 100 milioni ambazo zimewezesha wanafunzi hao kusoma katika mazingira mazuri.


Msaada huo umewezesha shule hiyo ya wasichana kupokea wanafunzi 750 wa kidato cha tano na sita.


Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, mhandisi Juma Hamsini amesema fedha hizo za Barrick pia zimesaidia ujenzi wa  matundu 21 ya vyoo .


“Tunaishukuru sana Kampuni ya Barrick Gold Mine na Rais Samia Suluhu kwa ufadhili huu umesaidia sana watoto wetu wa kidato cha tano na sita wa mchepuo wa Sayansi kupata shule ya kisasa" alisema.


Amesema, Halmashauri ya Jiji la Arusha imetoa Shilingi 100 Milioni kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kutengeneza madawati,vitanda na kununua vifaa vya kupikia na kuwaomba wadau mbalimbali waendelee kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia.


Amebainisha kuwa Jiji limeweka mikakati ya kutoa motisha kwa walimu wa ajira mpya ambapo wanawawezesha fedha za kujikimu kabla hawajapata mishahara.


Mkuu wa Shule hiyo Mwasiti Kinyau ameishukuru Kampuni ya Barrick Gold Mine kwa ufadhili wao mkubwa


"Tunawashukuru sana kwa msaada huo,pia niwashukuru Rais wetu Samia Suluhu ,Mkuu wa Mkoa was Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha na Mkurugenzi wa Jiji kwa usimamizi wao mzuri, na kwa mazingira haya sasa tunaomba kuongezewa walimu wengi zaidi,”amesema.


Kinyau alisema kwa saaa shule hiyo ina walimu 18 na baada ya kukamilika madarasa na mabweni yote katika mradi huo watakuwa na Uwezo was kupokea wanafunzi zaidi ya 300.




No comments: