TIGO Yawezesha Maonesho ya Wafanyabiashara Viwanja vya Makumbusho Jijini Arusha - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 12 December 2023

TIGO Yawezesha Maonesho ya Wafanyabiashara Viwanja vya Makumbusho Jijini Arusha

Mratibu wa Maonesho ya wafanyabiashara jijini Arusha Agustine Namfua akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kuhusu Maonesho ya wafanyabiashara yanayofanyika katika viwanja vya Makumbusho Jijini Arusha 

Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Daniel Mainoya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maonesho ya wafanyabiashara yanayofanyika katika viwanja vya  Makumbusho Jijini Arusha 



Na Andrea Ngobole, Arusha

maipacarusha20@gmail.com


Jumla ya wafanyabiashara na wajasiriamili 150 wanashiriki Maonesho ya wafanyabiashara na kongamano la Ujasiriamali Business  Summit linalofanyika viwanja vya Azimio jijini Arusha kuanzia Leo Jumanne December 12.



Mratibu wa Maonesho hayo Augustine Namfua amesema kuwa Maonesho bhayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara  hao kuuza bidhaa zaonkwa urahisi na pia kuwasaidia wanunuzi wa bidhaa mbalimbali kujipatia bidhaa kwa urahisi kipindi hiki Cha sikukuu za krismas na mwaka mpya.

Maonesho hayo yanayofahamika kwa jina Arusha Trade Fair 2023  ni ya awamu ya pili kufanyika katika viwanja hivyo na yanaanza Leo tarehe 12 - 17 Disemba 2023.


"Maonesho haya ni fursa kwa wananchi wa Arusha kujipatia mahitaji, huduma na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya sikukuu za krismas na mwaka mpya kwa Bei rafiki." Alisema Agustine 


Kabla ya Maonesho haya wafanyabiashara hao walishiriki Kongamano la biashara ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa na wataalamu ikiwemo Mikopo, Uwekezaji na Huduma za kifedha kidijitali toka kampuni ya mawasiliano ya Tigo ambao ndiyo wadhamini Wakuu wa Maonesho hayo.


Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Daniel Mainoya Amesema kuwa wao kama kampuni ya mawasiliano wanafuraha kuwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali kutumia huduma Bora za tigopesa kuuza na kununua bidhaa kwa urahisi.

Katika Maonesho hayo Tigo wameweka Banda ili kurahisisha huduma za kifedha kwa wafanyabiashara na wanunuzi kuweza kutoa na kuweka Pesa kwa tigopesa na pia kujishindia zawadi kemkem za msimu wa sikukuu maarufu kama Maguft Dabo Dabo


Amesema pamoja na Huduma za keep fedha pia katika Banda lao watakuwa wakiuza simu na vifaa vingine vya mawasiliano kwa Bei nzuri inayoendana na kampeni ya zawadi dabodabo.

No comments: