WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA RELI YA SGR KABLA YA KUANZA KUTUMIKA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 30 January 2024

WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA RELI YA SGR KABLA YA KUANZA KUTUMIKA

 

Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, Kamishna msaidizi wa polisi (ACP) Sebastian Mbuta, akizungumza na waandishi wa Habari 


Na: Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


Hujuma kwenye miundo mbinu ya Reli ya kisasa ya treni ya mwendo kasi(SGR) hata kabla ya kuanza kutumika imeendelea baadhi ya maeneo ya Ngerengere Mkoani Morogoro ambapo watu watatu wamekamatwa wakiwa na vipande 390 vya nondo za ukubwa wa milimita 16 zilizokuwa awali zimejengea uzio kuzuia kukatiza wanyama waharibifu ikiwemo Tembo.


Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, Kamishna msaidizi wa polisi (ACP) Sebastian Mbuta, amefika eneo la tukio na kujionea uharibifu huo, sambamba na kufika kituo cha Polisi Ngerengere kushuhudia nondo zilizokamatwa.


Aidha mkoani Dodoma nako amekamatwa mtu mmoja Elia Elias, (24), maeneo ya Makulu akiharibu miundo mbinu hiyo ya Reli kwa kubomoa nguzo nane za uzio wa SGR kwa kuzivunja kwa kutumia nyundo kubwa na kuchukua nondo zilizomo ndani yake kwaajili ya kwenda kuziuza kama vyuma chakavu.


Mwandishi wa habari hizi alifika  eneo la Ngerengere na kushuhudia nondo zilizowekwa katika uzio wa kuzuia wanyama waharibifu ikiwemo tembo, na ambazo treni ikianza safari zake, zitaunganishwa na umeme, zikiwa zimenyofolewa eneo moja hadi jingine, na kuacha uwazi mkubwa palipoondolewa vifaa hivyo ikilinganishwa na maeneo zilizo nondo kwa mpangilio sahihi.


Kamanda huyo wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, Kamishna msaidizi wa polisi (ACP) Sebastian Mbuta, akizungumza na vyombo vya habari amesema maeneo magumu watuhumiwa wamekuwa wakitumia maji kuyeyusha ardhi na kuwarahisishia kung'oa na kuacha mashimo.


ACP Mbuta amebainisha katika tukio la Ngerengere, tayari wamewatia mbaroni Florah Mbago, (39) mkazi wa Kiburumo Ngerengere na Juma Kijiti KItu(66) mkazi wa Mgudeni Ngerengereaa waliokutwa na vipande 17 vya nondo za ukubwa wa milimita 16, mali ya kampuni ya nchini Afrika Kusini ya Rubis, waliopewa kandarasi ya kujenga kilometa 16 za uzio huo wa kuzuia wanyamapori kuvuka upande mmoja kwenda mwingine na kuharibu reli.


Alibainisha mtuhumiwa mwingine Living Emmanuel(20) ambaye ni fundi wa kujenga uzio na mkazi wa Chamwino Ngerengere, yeye alikamatwa akiwa na vipande vya nondo vilivyokatwa 379, na upelelezi wa mashauri hayo unakamilishwa kwa haraka ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani,


Kamanda huyo wa Polisi Kikosi cha Reli, alisema wamefanya jitihada mbalimbali kuzuia uhalifu katika njia ya Reli kwa kushirikisha jamii kupitia mikutano mbalimbali ikiwemo ya ana kwa ana na kupitia vyombo vya habari, na kuahidi kuendelea kushirikiana na wananchi wanaotoa taarifa katika mapambano ya kuzuia vitendo vya uhalifu katika himaya ya Reli.


Alisema katika kipindi cha mwaka jana 2023 pekee, jumla ya watuhumiwa 97 waliweza kukamatwa kwa kufanya uhalifu kwenye himaya ya Reli, na watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani na wengi wao tayari wamehukumiwa, hivyo kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa ya vitendo vya kiuhalifuili kuhakikisha mali za shirika la Reli na miundo mbinu yake inakuwa salama.


“Adhabu wanazopewa sio ndogo, wengine wanafungwa hadi miaka 20 na ndio maana tukiwakamata tunawafikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria, na wapo wengine huwa tunawapeleka kwa makossa ya uhujumu uchumi, Reli hii ikianza kazi kila mtanzania atafaidika na reli hii ya kisasa, nizidi kuwaomba wananchi waguswe kwa dhati kutoka moyoni kuwa hii reli ni ya kwetu," alisrma.


Aliwataka mwaananchi atakayeona hujuma zozote kwenye miundo mbinu ya Reli atoe taarifa kwa vyombo vya dola ama viomgozi kwenye maeneo yao.


Kwa upande wake Meneja Mradi wa ujenzi wa uzio huo wa kuzuia wanyamapori waharibifu wakiwemo tembo kwenye SGR kipande cha Ngerengere, Petter de Lange kutoka kampuni ya Rubis ya nchini Afrika ya kusini, alieleza kusikitishwa na kitendo kinachofanywa na baadhi ya watanzania kuhujumu mali yao wenyewe, kwani reli hiyo ikikamilika, italeta manufaa ya kiuchumi kwa watanzania wenyewe.


Alisema reli hiyo ni mahususi kuzuia mapito ya wanyamapori,eneo kla Kidugalo, baada ya kufanya utafiti na kubaini eneo hilo ni mapito ya wanyamapori wakiwemo Tembo, na nia mahususi ni kulinda reli hiyo isipate madhara yeyote ikiwemo ajali kwa kugongana na mnyama kama Tembo na wengine.


Makosa mbalimbali ambayo watuhumiwa walikamatwa ndani ya himaya ya Reli na wengine kufikishwa mahakamani katika kuipindi cha mwaka jana na mwaka juzi, kwamujibu wa ACP Mbuta, ni pamoja na wizi wa vyuma vya reli aina ya sahani (Sole Plate),chuma aina ya Coprini,vipande vya nondo milimita nane na 16, kukamatwa na madawa ya kulevya ikiwemo bangi na mirungi, mabomba ya urefu wa futi kumi ya kujengea madaraja ya Reli,mabomba ya maji, mipira ya kusambaza maji, mifuko ya mbolea kwaajili ya vilipuzi, wizi pamoja na uharibifu wa miundo mbinu.


No comments: