WANAFUNZI ISHIRINI WAPATIWA VIFAA VYA SHULE USANGULE MALINYI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 17 January 2024

WANAFUNZI ISHIRINI WAPATIWA VIFAA VYA SHULE USANGULE MALINYI

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


Wanafunzi ishirini (20) wa shule ya msingi Ifungila iliyopo  kata ya Usangule Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro, wamepatiwa vifaa mbalimbali vya shule ambavyo ni sale za shule, madaftari na kalamu ili kuweza kumudu vyema masomo yao.


Utoaji wa vifaa hivyo umekuja baada ya wanafunzi hao kurudi shule bila vifaa vipya wakidai walezi wao wameshindwa kuwanunulia kutokana na hali duni ya maisha.


Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Michael Rasha ambaye ni Polisi Kata wa Kata hiyo ya Usangule akizungumza na walimu pamoja na Wanafunzi wakati wa kukabidhi vifaa hivyo,  amesema, Kitendo cha wanafunzi hawa kurudi shuleni mwaka mpya wakiwa na vifaa vya mwaka uliopita kimemsikitisha na kumgusa.


"Hili jambo limepelekea nichukue  maamuzi ya kununua na kuwapelekea hivi vifaa walau viwasaidie Sisi kama jamii tunapaswa kuwasaidia wenye mahitaji,"alisema.


Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Henry Mwangake anaye ihudumia Kata jirani na Usangule amewataka wanafunzi hao kutumia fursa hiyo kusoma kwa bidii ili waje kuwa msaada kwa familia zao.


Polisi Kata hao kwa ujumla wao walitumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa Wanafunzi namna ya kujilinda na vitendo vya Ukatili, maeneo ha kutoa taarifa pamoja kulindana wao kwa wao.


Aidha wanafunzi hao walifundishwa miladi ya Polisi Jamii ikiwemo Usalama wangu kwanza, Familia yangu haina muhalifu Pamoja na kauli mbiu ya Polisi Jamii.


Mwalimu Ally Makambi akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa shule hiyo, ameshukuru kwa msaada huo uliotolewa na Askari hao na kuitaka jamii kuiga mfano huo kwani kuna wanafunzi wengi ambao wanauhitaji wa vifaa vya shule katika shule hiyo.


Makambi alisema ni vyema kama kuna mdau yoyote anaweza kufika na kutoa alicho jaaliwa ili wanafunzi wote wawe na hali inayo fanana.


No comments: