WAWEKEZAJI ARUSHA WAPONGEZA SERA BORA ZA UWEKEZAJI NCHINI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 18 January 2024

WAWEKEZAJI ARUSHA WAPONGEZA SERA BORA ZA UWEKEZAJI NCHINI

 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Hanspaul, Satbir Singh akizungumza na waandishi wa Habari


Baadhi ya magari yanayotumia umeme yakiwa tayari Kwa shughuli za utalii


Na Elinipa Lupembe, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Wawekezaji wa Kampuni ya  Hanspaul inayomiliki Kiwanda cha kuunganisha magari maalum kwa ajili ya shughuli za Utalii mkoani Arusha, wameipongeza na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwa na Sera bora zinazovutia wadau kuwekeza nchini.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Hanspaul, Satbir Singh Hanspaul kiwandania hapo, hakusita kuipongeza Serikali,  kwa kuwa na Sera nzuri zinazosababisha mazingira rafiki kwa wawekezaji nchini. 


Ameweka wazi kuwa, kupitia Kituo cha Uwekezaji cha Taifa,  imeweka mazingira rafiki yanayowezesha wawekezaji wa ndani kufanyakazi kwa kushurikiana na sekta zote, zaidi mazingira yanayoruhusu na kuvutia wawekezaji kutoka nje ya nchi kuwekeza Tanzania.


"Kiwanda chetu tunatengeneza magari yanayotumia umeme na yameanza kutumiwa na watalii, tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia,  Tamthilia ya Royal Tour imeleta watalii wengi nchini, watalii ambao wengi wanavutiwa kuwekeza Tanzania, huku TIC ikifanyakazi kubwa ya kuwaunganisha wawekezaji wakubwa, mashirika na watu binafsi".Amesema Satbir Singh


Kutokana na amani na utulivu  wa kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini, umewezesha wazawa na hata wageni kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa uhuru, unaokwenda sambamba na kukuza uchumi wa nchi.


Awali, Meneja Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Felix John amesema kuwa, TIC inafanya kampeni ya kitaifa kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani, ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu zana ya uwekezajia pamoja ja kubadili fikra na mtazamo wa watanzania kwamba wawekezaji ni wageni kutoka nje ya nchi.


"Kampeni hiyo ni muhimu kwa watanzania, inayolenga pia kuwahamasisha watanzania,  kushiriki kikamilifu kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na kuchangamkia fursa zilizoko" Amebainisha John


Hata hivyo, ameaeka wazi kuwa, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, kwa kushirikiana na TIC, wameshusha kiwango cha fedha za uwekezaji hasa kwa wazawa kutoka Dola za Kimarekani 100,000 hadi kufikia 50,000 sawa na Sh.milioni 125, kwa lengo la kuwavutiwa wawekezaji wa ndani kuwekeza na kusajili miradi.



No comments: