Balozi Dkt Pindi Chana awataka waendesha mashtaka Nchini kutumia miongozo ya Makosa ya wanyamapori Kudhibiti ujangili - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 19 February 2024

Balozi Dkt Pindi Chana awataka waendesha mashtaka Nchini kutumia miongozo ya Makosa ya wanyamapori Kudhibiti ujangili


WAZIRI wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza na wapelelezi pamoja na waendesha mashtaka katika warsha ya hakijinai iliyoenda sambamba na uzinduzi wa miongozo miwili ya usimamizi wa makosa ya wanyamapori, mazao ya misitu na uvuvi haramu 


WAZIRI wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana akizundua miongozo miwili ya usimamizi wa makosa ya wanyamapori, mazao ya misitu na uvuvi ili kudhibiti ujangili na uvuvi haramu nchini Tanzania

WAZIRI wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana pamoja na Viongozi Toka ofisi ya DPP wakionesha miongozo miwili ya usimamizi wa makosa ya wanyamapori, mazao ya misitu na uvuvi ili kudhibiti ujangili na uvuvi haramu nchini Tanzania 


Na: Andrea Ngobole, MAIPAC


maipacarusha20@gmail.com


WAZIRI wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana amezindua miongozo miwili ya usimamizi wa makosa ya wanyamapori, mazao ya misitu na uvuvi ili kudhibiti ujangili na uvuvi haramu nchini Tanzania.


Amezindua miongozo hiyo jijini Arusha Leo February 19 wakati wa hafla ya uzinduzi wa miongozo ya kushughulikia kesi za uvuvi haramu, ujangili wa wanyamapori na uvunaji misitu katika mkutano wa mafunzo  kwa wapelelezi na waendesha mashtaka nchini Dkt.Chana amesema miongozo hiyo itawasaidia wadau wa kesi hizo, kuziendesha kwa haki na kuleta manufaa kwa rasilimali nchini.


"Jukumu la kulinda rasilimali zetu ni letu sisi wenyewe hivyo naamini wapelelezi na waendesha mashtaka kwa sasa mtasaidia kukomesha ujangili wa wanyamapori wetu, uvuvi haramu kwenye maziwa na bahari, lakini pia kukomesha uharibifu wa misitu yetu,"alisema.


Aidha alisema rasilimali zilizopo nchini  zinachangia pato la Taifa na fedha hizo zinafanikisha kuendeshanshughuli mbalimbali za maendelo.


Amesema baada ya uzinduzi huo anawatahadharisha wanaojihusisha na ujangili wa rasilimali za Taifa kuacha kwani wadau wa maeneo hayo wamejipanga vizuri kuhakikisha wana komesha tabia hizo.


Dkt. Chana amesema Taifa haliwezi kuacha baadhi ya watu wakiendelea kuvuna rasilimali za nchi kwa manufaa yao peke yao, bila kuafuata sheria  ni lazima wadhibitiwe.


Awali akimakaribisha mgeni rasmi Balozi Dkt Pindi Chama, Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Sylvester Mwakitalu alisema uzinduzi wa miongozo hiyo ina manufaa makubwa kwa maliasili nchini.


"Tumeona tuhuhishe muongozo wa usimamizi wa wanyamapori na misitu na muongozo wa mazao ya uvuvi, sababu tumeona tusipokua makini katika kulinda rasilimali zetu kama bahari na maziwa yatabaki tupu kutokana na uvunaji haramu wa mazao haya unavyozidi kushamiri,"alisema


Alisema kuna wakati makosa hayo yanafanywa kwa kupanga  kitaifa na kimataifa, hivyo kupitia miongozo hiyo itawasaidia kudhibidi uhalifu huo ndani na nje ya nchi.



Pia katika ukusanyaji wa ushahidi  wa makosa hayo kupitia miongozo hiyo itasaidia  kufanywa kisanyansi, teknolojia na kielekroniki na mafunzo hayo yatatolewa kwa wadau wa sekta hiyo nchi nzima Kwa  waendesha mashtaka Toka Taasisi za utalii kama TANAPA, TAWA, NCAA, TFS, POLISI na TAKUKURU

Kaimu Mkurugenzi wa Mashataka nchini (DPP) Javelin Rugaihuruza alisema  ofisi ya DPP imeona kuna umuhimu wa kuandaa mafunzo hayo ili kufundisha wadau mbinu mpya zianazotumiwa na wahalifu wa rasilimali nchini  kwa manufaa ya Taifa.


Kwa upande wake Katto Wambura kutoka Umoja wa Mataifa Ofisi ya Madawa na Uhalifu (UNODC)  ambao ndiyo wameandaa miongozo hiyo na kuwezesha mafunzo Kwa waendesha mashtaka na wapelelzi nchini alisema watatengeneza APP itakayowezesha  kuisoma miongozo hiyo kwenye simu, Pamoja na kusoma miongozo ya nchi zingine.

####

No comments: