JESHI LA POLISI LINAMSAKA LARINYONI SAITOTI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKE WAKE USIKU WA MANANE LOLIONDO. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 15 February 2024

JESHI LA POLISI LINAMSAKA LARINYONI SAITOTI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKE WAKE USIKU WA MANANE LOLIONDO.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo 


Na:Mwandishi wetu, MAIPAC 


maipacarusha20@gmail.com


Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamsaka Larinyoni Saitoti Parmeres (28) mkazi wa kijiji cha Lopuluni kitongoji cha Lopoluni A tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Kwa tuhuma za kumuua mke wake Nang'obukule Ikayo Mbalala (20) kwa kumpiga na rungu Kisha kumkata na kitu chenye ncha kali maeneo mbalimbali ya mwili wake na kutokomea kusikojulikana.


Akizungumza na maafisa wa  shirika la Mimutie Women Organization  linalopambana na kupinga ukatili kwa wanawake wilayani Ngorongoro, wapofika eneo la tukio mwenyekiti wa kijiji cha Lopoluni, Daniel Kurutut amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jumatano ya Februari 14 2024 ambapo mtuhumiwa baada ya kutenda ukatili huo alitoroka na wao kwa kushirikiana na jeshi la polisi watahakikisha anapatikana na kufikikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma hizo.


Mashuhuda waliogundua ukatili huo baada ya kufika nyumbani kwa marehemu akizungumza na maafisa wa  shirika hilo la Mimutie, Tomboy Ole Sayori amesema majira ya saa 12 asubuhi mtuhumiwa baada ya kutekeleza unyama huo alichukua hatua ya kumpeleka mtoto wake wa kike mwenyewe mri wa miaka (2) waliyekuwa wakiishi nae kwa mama mzazi wa mtuhumiwa.


Amesema baada ya kumfikisha mtoto huyo alimuacha njee huku yeye akitokomea kusikojulikana ndipo mama wa mzazi wa mtuhumiwa alipogundua uenda kuna tukio limetendaka lisilo la kawaida baada ya kumuona mjukuu wake akiwa ametapakaa damu katika nguo alizokuwa amezivaa.


Tomboy amesema kuwa baada ya mama wa mtuhumiwa kuona hivyo ndipo alipoenda kumuita yeye na kumueleza, huku akichukua hatua ya kwenda kwa marehemu na alipofika na kuingia ndani aligundua marehemu ameuwawa kikatili na mume wake akiwa na majeraha ya kupigwa na rungu (maarufu namba tisa kwa umasaini) maeneo ya kichwani  pamoja na kuwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya mbalimbali ya mwili wake.


Kwa upande wake Bwn Isaya Seki mkazi wa kijiji icho akizungumzia tukio hilo amesema mtuhumiwa amekuwa akitishia familia yake kutaka kuua kwani mke mkubwa aliondoka kutokana na kuhofia kuuawa na hata alikuwa akimtishia mama yake mzazi kutaka kumuawa.


Alipotafutwa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo kuzungumzia kwa undani na chanzo cha tukio hilo simu yake iliita bila mafanikio huku mtuhumiwa akiwa bado hajapatikana.


Hili ni tukio la pili kutokea wilayani Ngorongoro ndani ya wiki moja kwani shirika la Mimutie liliripoti tukio lingine la kikatili katika kijiji cha Malambo mnamo tarehe 06/02/2024 mwanaume mmoja kwa jina la Lanyori Mathayo (25) alimuua mke wake kwa kipigo baada ya kugoma kuishi nae.

No comments: