KESI INAYOPINGA WATU KUSHTAKIWA KWENYE MAHAKAMA ZISIZO NA MAMLAKA YASIKILIZWA LEO JIJINI DARESALAAM - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 12 February 2024

KESI INAYOPINGA WATU KUSHTAKIWA KWENYE MAHAKAMA ZISIZO NA MAMLAKA YASIKILIZWA LEO JIJINI DARESALAAM

 

Mratibu wa mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania Wakili Onesmo Olengurumwa

Na: Mwandishi wetu, MAIPAC


maipacarusha20@gmail.com


Kesi ya Mtetezi mahiri wa Haki za Binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Rufaa Na. 165 ya mwaka 2021 imesikilizwa leo tarehe 12.02.2024 katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania,jijini Dar es Salaam mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufani Mhe. Jaji Sehel, Mhe. Jaji Kente, na Mhe. Jaji Masoud saa 3:00 asubuhi


Rufaa hiyo inatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam uliotolewa mwaka 2020 ambapo Mahakama kuu ilitupilia mbali kesi hiyo ambayo ilikuwa inapinga vifungu vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai vinavyoruhusu washtakiwa kushtakiwa kwenye mahakama za chini ambazo hazina mamlaka ya kusikiliza kesi hizo (committal Proceedings). 


Vifungu vinavyolalamikiwa na wakili Olengurumwa ni namba 178, 243, 244, 245, 246, 247, 248, 249, 250, 256, 257,258 na 259 vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. 


Katika Mahakama Kuu Wakili Olengurumwa aliitaka mahakama itoe amri ya Kubatilisha vifungu hivyo vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwasababu vinakiuka Katiba na haki za binadamu kwa mfano haki ya kusikilizwa kwa usawa, usawa mbele ya sheria n.k. ambazo zipo katika Ibara ya 13 (1) (2) na (6) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.


No comments: