SAKATA LA KUACHIWA WATUHUMIWA WATATU WA UJANGILI MENO YA TEMBO LATUA KWA MSAJILI WA MAHAKAMA MANYARA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 6 February 2024

SAKATA LA KUACHIWA WATUHUMIWA WATATU WA UJANGILI MENO YA TEMBO LATUA KWA MSAJILI WA MAHAKAMA MANYARA




Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Manyara Mpepo Bernard kati kati akiwa na maafisa wengine wa mahakama mkoa Manyara.



Mwandishi wetu, Babati.


maipacarusha20@gmail.com


Sakata la kuachiwa huru Watuhumiwa watatu waliokamatwa na vipande sita vya meno ya Tembo limetua kwa msajili wa Mahakama Kanda ya Manyara.


Watuhumiwa hao,Bashiru Ally, Daniel Gwandu na Frank Gadiye, waliachiwa huru na Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama ya mkoa Manyara Mariam Lusewa kwa sababu za kukosekana ushahidi wa kuwatia hatiani.


Kutokana na hukumu hiyo. Ambayo ilitolewa Novemba 20 mwaka Jana, imepingwa na Ofisi ya Mashitaka (DPP) mkoa Manyara na Ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) ambao waliwasilisha notisi ya kukata rufaa lakini kwa zaidi ya miezi miwili Sasa wameshindwa kupata mwenendo wa shauri hilo ili waendelee na rufaa.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara, Mpepo Bernard amesema Ofisi yake ilikuwa haina malalamiko juu ya shauri hilo.


Hata hivyo ameagiza ofisi ya DPP kupatiwa mwenendo wa mashitaka kwa ajili ya kukata rufaa ifikapo  Februari 7, mwaka huu.


"Kama kwa muda wote huu hawajapata mwenendo wa kesi ni tatizo lakini nimeagiza uchapwe haraka na kukabidhiwa wakata rufaa"amesema


Amesema kwa kawaida mwenendo wa kesi ulipaswa kuwa tayari ndani ya mwezi mmoja.


"Jumatano (kesho) mwenendo wa kesi itakuwa tayari kwani bado muda wa kukata rufaa upo kwa kuwa tayari waliwasilisha notisi ya kukata rufaa"alisema.


Awali Mwendesha mashitaka wa TAWA, Getrude Kariongi kwa kushirikiana na DPP wamepeleka notisi ya kukata rufaa lakini tangu mwezi Novemba walikuwa hawajapata mwenendo wa kesi.


"Kuna changamoto hizi kesi za ujangili kwani Watuhumiwa wakiachiwa muda ukiwa mrefu kuwapata ni shida kwani wengi hukimbia ndio sababu tumekuwa tulitaka mwenendo wa kesi ili tukate rufaa"alisema


Alisema Upande wao DPP na TAWA wanaamini wana ushahidi wa kutosha kuendelea na shauri hilo ili kukomesha matukio ya ujangili.


Watuhumiwa hao walioachiwa huru walikamatwa Machi 3 mwaka Jana, wakiwa na vipande sita vya meno ya Tembo eneo la njiapanda Madunga, wilayani Babati mkoa wa Manyara.


Meno hayo yalikuwa na thamani ya sh 137,910,300 milioni na yalikuwa yakibebwa kwenye viroba kusafirisha ambapo pia pikipiki zilizokuwa zimebeba meno hayo zilikamatwa.

No comments:

Post a Comment