Vikundi 10 vya Kijiji cha vilima vitatu vyapatiwa mafunzo ya elimu ya fedha - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations
Wednesday 7 February 2024

Vikundi 10 vya Kijiji cha vilima vitatu vyapatiwa mafunzo ya elimu ya fedha

 


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo waliokaa katikati akiwa na Mkurugenzi wa Chemchem Association Bi. Fabian Bausch kushoto na kulia ni Meneja Mkuu wa Chemchem Association Clever Zullu katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa vikundi 10 vilivyomo pembezoni mwa Jumuiya ya Hifadhi Burunge 


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo akifungua warsha ya siku tatu Kwa Viongozi wa vikundi 10 vilivyomo pembezoni mwa Jumuiya ya Hifadhi Burunge 


Mkurugenzi wa Chemchem Association Bi Fabian Bausch akizungumza na Viongozi wa vikundi 10 Toka vijiji vinavyozunguka Jumuiya ya Hifadhi Burunge 

Meneja Mkuu wa Chemchem Association Clever Zullu akizungumza na Viongozi wa vikundi 10 vilivyomo pembezoni mwa Jumuiya ya Hifadhi Burunge


Na: Andrea Ngobole, Babati


maipacarusha20@gmail.com


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo  amewahamasisha Viongozi wa vikundi 10 vilivyomo katika eneo la jumuiya ya  Hifadhi ya Wanyamapori ya  Burunge kuhifadhi kumbukumbu zao za fedha Kwa usahihi ili kuepusha migogoro itakayosababisha vikundi hivyo kuvunjika.


Ameyasema hayo Leo February 7 wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu Kwa Viongozi wa vikundi hivyo, iliyoandaliwa na Taasisi ya Chemchem Association inayofanya shughuli za uhifadhi katika Jumuiya ya Hifadhi Burunge iliyopo mkoani Manyara.


Amesema kuwa baadhi ya mambo yanayosababisha vikundi kuvunjika ni pamoja na kuto  kutunza kumbukumbu Kwa usahihi na kutumia fedha za kikundi bila utaratibu.

Amewataka Viongozi hao kuto kuhifadhi fedha majumbani na badala yake kufungua akauti ya kikundi bank kulingana na sera ya fedha ya jamii ya Mwaka 2019 inayotaka kila kikundi kuwa na akaunti ya benki.


"Serikali inathamini sana vikundi vya kuweka akiba na kukopa kwani vikundi hivi vinachochea maendeleo ya jamii hivyo Viongozi wa vikundi mnapaswa kuwa waaminifu Kwa pesa za kikundi ili kujenga Imani Kwa wanakikundi." alisema Mkurugenzi huyo.


Awali akimakaribisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Babati, Meneja Mkuu wa Chemchem Association Clever Zullu amesema kuwa wanajivunia sana kuwezesha vikundi hivyo Kwa miaka 7 Sasa kukopesheka na kuleta faida Kwa jamii ya vijiji hivyo pia furaha Yao ni kuona matunda ya uhifadhi unaoongozwa na wananchi wenyewe yanakuwa na manufaa makubwa.


Amevitaja vikundi 10 vinavyosimamiwa na Chemchem Association Toka mwaka 2017 mpaka Sasa kuwa ni Upendo -B, Marewa, Kigogoni, Datoga, Wacheda,Keja, Esinyati, Mdorii, Upendo -A na Mang'oo ambapo Viongozi wa vikundi hivyo watapatiwa mafunzo ya siku tatu ili kuendana na Sera ya Community Microfinance ya 2019 ambavyo vitasajiliwa na kutambuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Babati.


Mkurugenzi wa Chemchem Association Bi Fabian Bausch amesema kuwa Umoja  na mshikamano kati ya vikundi vya kuweka na kukopa vimewezesha kuwakwamua kiuchumi wakazi wa vijiji kumi vinavyozunguka Jumuiya ya Hifadhi Burunge.


Amesema wakati wanaanzisha vikundi hivi mwaka 2017 Kwa kila Kijiji jamii haikuwa na uelewa mkubwa juu ya kuwa na vikundi vya kuweka na kukopa lakini Kwa Sasa Dunia nzima inafahamu shughuli za uhifadhi zinazofanywa Juhibu na kuwavutia wageni wengi wanaokuja kutali na kuongeza fedha nyingi za kigeni.


Kupitia fedha hizo za uhifadhi na utalii wa picha Chemchem Association inarejesha Kwa jamii Kwa kusaidia katika sekta za elimu, Afya na mazingira.

Vikundi hivyo kumi vimekuwa vikilelewa na Chemchem Association Toka mwaka 2017 ambapo warsha hiyo itawasaidia kuweza kufungua akaunti za vikundi hivyo Benki ya NMB ili kuendana na matakwa ya sera ya fedha za jamii na uma ya Mwaka 2019 kuwekwa katika akaunti ya benki ili kuwa  salama.


No comments: