BODI YA CHAMA CHA USHIRIKA CHAPAKAZI KUFADHILIWA ZIARA YA MAFUNZO MTWARA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 4 March 2024

BODI YA CHAMA CHA USHIRIKA CHAPAKAZI KUFADHILIWA ZIARA YA MAFUNZO MTWARA

 






Na: Mwandishi wetu, Maipac Kibiti



MWENYEKITI wa Chama Kikuu Cha Ushirika Mkoa wa Pwani Mussa Mng'elesa ameahidi kupeleka bodi ya chama Cha Ushirika cha Msingi Chapakazi katika mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kujifunza.

Mng'elesa amesema ahadi hiyo kwa Chapakazi ambacho kipo Bungu Wilaya ya Kibiti imetokana na namna kinavyofanya vizuri katika kazi zake tangu kuanzishwa 

Amesema Chapakazi ni kati ya vyama 10 Bora kitaifa lakini pia limekuwa kikifanya vizuri kwenye suala la mapato na matumizi na kupata hati safi jambo ambalo bodi ikienda ziara za mafunzo kutakuwa na maboresho zaidi.

Akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika Bungu, Mwenyekiti huyo alisema vyama vya Ushirika ni uchumi hivyo vinatakiwa kuwa na wanachama wakulima na si wanasia.

Mrajisi msaidizi Mkoa wa Pwani Abillahi Mutabazi amesema katika ya vyama vya Ushirika vya ufuta na korosho 98 kwa mkoa huo havizidi kumi vyenye hati inayorishisha.

Amelekeza chama hicho kuongezea idadi ya wanachama sambamba na kuhakikisha wanajenga ghala na ofisi yao na kuachana na utaratibu wa kupanga.

Katibu wa Chapakazi Hassani Tinge amesema  katika msimu wa mwaka 2023/2024 chama hicho kimepokea kipima unyevu na ubora pamoja na mashine ya kisasa ya kupulizia korosho kutoka CORECU.

Tinge amesema pia chama hicho kimefanikiwa kuongeza ubora wa korosho ambapo kg 676,543 zilizouzwa zilikuwa daraja la kwanza na kg 178,344 zilikuwa daraja la pili huku zilizo chini ya ubora zikiwa ni kg 21,971.

Amesema chama hicho kina malengo ya kujenga ofisi, ghala la kuhifadhia mazao sambamba na ukumbi wa sherehe.


No comments: