Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika hilo Mussa Nassoro Kuji Juma akihitimisha kikao kazi hicho. |
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Mhandisi Mshauri, Dkt. Richard John Matolo, akizungumza katika kikao kazi hicho. |
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye kikao kazi hicho. |
Afisa Uhifadhi Mkuu - TANAPA ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, Catherine Mbena, akizungumza katika kikao kazi hicho. |
Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Herman Batiho akiwa kwenye kikao kazi hicho. |
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Jully Lyimo akiwa kwenye kikao kazi hicho. |
Na Mwandishi Wetu
maipacarusha20@gmail.com
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan, limeibuka na ongezeko kubwa la Watalii na mapato, hivyo kukidhi malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) ya 2020 – 2025.
Katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM iliyotolewa Agosti 2020, inaelekeza kwamba katika sekta ya Utalii, hadi ifikapo mwaka 2025, idadi ya watalii nchini ifikie milioni 5 na mapato yafikie dola za kimarekani Bilioni 6 kwa mwaka.
Akieleza mafanikio katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dk. Samia, katika Kikao Kazi baina yake na Wahariri wa habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika Jijini Dar es Salaam, leo Machi 21, 2024, Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika hilo Mussa Nassoro Kuji Juma, amesema katika kipindi hicho TANAPA imeibuka na ongezeko la mapato kutoka Sh. Bilioni 174.7 (Sh.174,715,158,494 (2021/2022) hadi kufikia Sh.Bilioni 337.4 (Sh. 337,424,076,896) mwaka 2022/2023.
Alisema ongezeko hilo ni sawa na ongezeko la Sh. Bilioni 162.7 (Sh.162,708,918,402) ambayo ni asilimia 94.
Aidha, kwa mwaka wa fedha 2023/2024 (Julai 2023 hadi Machi 19, 2024) TANAPA imekusanya Sh.Bilioni 340.1 (Sh. 340,101,108,465) ikilinganishwa na matarajio ya kukusanya Sh. Bilioni 295.4 (Sh 295,466,811,506) hadi Machi 2024, kiasi ambacho kikiwa ni ongezeko la Sh. Bilioni 44.6 (Sh. 44,634,296,959) ambazo ni sawa na asilimia 15 na Shirika likiwa na matarajio ya kukusanya kiasi cha Sh. Bilioni 382.3 (Sh. 382,307,977,497) hadi Juni 2024.
Kamishna Juma, alisema mapato hayo ya sasa yanazidi mapato ya Sh. Bilioni 282 (Sh. 282,450,446,103)
yaliyokusanywa mwaka 2018/2019 kabla ya janga la UVIKO – 19, ambayo yalikuwa ndio kiwango cha juu cha mapato katika Shirika.
"Ongezeko hili la watalii na mapato linaenda sanjari na malengo ya Ilani ya Chama Chama cha Mapinduzi 2020 – 2025, inayoelekeza idadi ya watalii nchini kufikia milioni 5 na mapato ya dola za kimarekani Bilioni 6 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025", akasema Kamishna Juma.
Alisema, pia kumekuwepo na kuchipuka kwa masoko mapya ya utalii yenye idadi kubwa ya watalii ambapo inatoa uhakika wa kuendelea kupokea watalii wengi kufika kutembelea Hifadhi za Taifa na kwamba masoko hayo mapya ni pamoja na China, Urusi, Ukraine, Poland, Jamhuri ya Czech na Israeli.
Kamishna Juma alieleza mafanikio lukuki katika kipindi hicho cha miaka mitatu ya Rais Dk. Samia.
No comments:
Post a Comment