AJALI YA MOTO BAADHI YA VIBANDA STANDI YA MSAMVU VYATEKETEA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 24 July 2024

AJALI YA MOTO BAADHI YA VIBANDA STANDI YA MSAMVU VYATEKETEA

 





Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


AJALI ya Moto ambao chanzo chake hakijajulikana umeteketeza baadhi ya vibanda vya wafanyabiashara vilivyopo standi ya  mabasi Msamvu Manispaa ya Morogoro.


Wakizungumza baada ya ajali hiyo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema moto huo ulianza majira ya saa tatu usiku ya julai 23,mwaka huu ambapo walianza jitahada za kuuzima pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi la Zima moto na uokoaji.


Shuhuda Mohamedi Ally mkazi wa Manispaa  Morogoro alisema askari wa Zimamoto walifika kwa wakati na kufanikiwa kuudhibiti moto huo.


Naye Fredy Makungu mashuhuda alisema miti ulikuwa mkubwa na inaonekana kusababisha hasara kwa wenye vibanda hivyo, na aliishukuru Jeshi la zima moto kwa kuwezesha kuzima moto.


Akizungumzia moto huo mwenyekiti wa mtaa wa White house,Kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro ilipo stendi hiyo Said Daudi alisema bado hawajajua hasara iliyosababishwa na moto huo wanachosubiri ni tathimini itakayofanyika.


Operesheni ofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Morogoro mrakibu msaidizi Daniel  Myalla alisema wamefanikiwa kuudhibiti moto huo ambao haujaleta madhara kwa binadamu zaidi ya bidhaa za wafanyabiashara Hao.


Mwisho.

No comments: