AFUNGWA MIAKA 30 JELA KWA KOSA LA KUBAKA NA KUMLAWITI BINTI MLEMAVU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 24 July 2024

AFUNGWA MIAKA 30 JELA KWA KOSA LA KUBAKA NA KUMLAWITI BINTI MLEMAVU

 





Na: Epifania Magingo, Babati 


maipacarusha20@gmail.com 


Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara imemtia hatiani Kijana Ramadhani Iddi Kipusa (19) kutumikia kufungo cha miaka 30 jela  kwa makosa mawili ya kubaka na kumlawiti binti mlemavu (Bubu) huku akitakiwa  kulipa fidia ya Shilingi laki 5 kwa kila kosa.


Kesi ya Jinai namba 5310/ 2024 Jamuhuri dhidi ya Ramadhani Iddi Kibusa, hukumu yake imesomwa na hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya  Babati Martin Masao ambapo Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na Jamuhuri dhidi Kijana huyo, Mahakama hiyo imejiridhisha  kuwa Ramadhani Iddi Kipusa alimbaka na kumlawiti binti huyo.(jina limehifadhiwa) 


Aidha , Hakim Martin Masao amesema mtuhumiwa Ramadhani Iddi Kipusa (19) ametiwa hatiani Kwa makosa mawili ya kubaka na kulawiti ambapo Kwa kosa la kubaka mtuhumiwa ametenda kosa hilo kinyume cha kifungu Cha sheria namba 130 (1) na kifungu kidogo Cha 2 (a)  ikisomwa sambamba na kifungu 131(1) ambacho kinatoa adhabu,  na kosa la pili la kulawiti kinyume cha kifungu cha sheria namba 154 (1)(a) Cha sheria ya kanuni za adhabu sura namba  6 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.


Kijana Ramadan Iddi Kipusa amehukumiwa kwenda jela kutumikia kufungo cha miaka 30 Kwa Kila kosa ambapo atatumikia Kwa wakati Mmoja na ametakiwa kulipa fidia ya shilingi laki 5 Kwa Kila kosa.


Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Mkoa wa Manyara Chema Maswi amesema kwa upande wa Jamuhuri wameridhishwa na hukumu hiyo na kwamba itakuwa fundisho Kwa watu wengine wenye tabia za kufanya matukio ya ukatili wa kijinsia.


Imeelezwa kuwa June 2 ,2024 Kijana Idd Kipusa alitekeleza kitendo hicho Cha ubakaji na kumlawiti binti huyo akiwa nyumbani kwa wazazi wake anapoishi Magugu Wilayani Babati Mkoani Manyara.

No comments: