KARATU WATAKIWA KUONGEZA ULINZI WA MTOTO DHIDI YA UKATILI WA JINSIA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 19 July 2024

KARATU WATAKIWA KUONGEZA ULINZI WA MTOTO DHIDI YA UKATILI WA JINSIA

Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Arusha Cecilia Daniel Pareso akizungumza na wanafunzi wa secondary ya Upper Kitete wilayani Karatu mkoa wa Arusha




 Na: Mwandishi Wetu maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Jamii  wilayani Karatu mkoani Arusha imetakiwa kuwalinda watoto wa pande zote  mbili bila kuwatenga kwa jinsia kutokana na mabadiliko ya kidunia.


Hayo yamesemwa na mbunge wa viti Maalum mkoa wa Arusha Cecilia Daniel Pareso wakati akizungumza kwa nyakati tofati na wananchi katika mikutano yake ya hadhara ya kukagua miradi ya maendeleo ndani ya wilaya hiyo pamoja na kusikiliza kero za wananchi ambapo pia alitembelea baadhi ya shule na kuzungumza na wanafunzi.


Cecilia Amesema kuwa zamani ulinzi wa mtoto jamii ilijikita zaidi kwa watoto wa kike pamoja na serikali lakini kwa Sasa matukio yamekuwa mengi kwa pande zote mbili hivyo wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao kwa kutoa maadili na kuwaasa watoto wao dhidi ya mambo ya kidunia.


"Zamani tulikuwa tunawalinda zaidi watoto wa kike lakini Sasa watoto wote wanatakiwa ulinzi zaidi kwani matukio ya ukatili yamekuwa mengi na vijana wetu bila kuwa karibu nao tutakosa jamii imara yenye maadili sahihi,naomba tuwe karibu na vijana wetu wazazi na walezi". Amesema Cecilia.


Akizungumza na wanafunzi Cecilia aliwaasa wanafunzi kutosoma ilimradi wanaenda shule Bali wasome kwa kuweka nia na kufikia ndoto zao,*Nawaasa msisome ilimradi someni kwa malengo bila kuruka hatua zote zinazotakiwa katika maisha*Amesema Cecilia.

No comments: