TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YAPOKEA MALALAMIKO YA WANANCHI MOROGORO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 19 July 2024

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YAPOKEA MALALAMIKO YA WANANCHI MOROGORO

 




Na: Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imepokea malalamiko kuhusu athari walizozipata wananchi wa eneo la Block five mtaa wa Yespa kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro baada kujengwa tuta la reliI ya Kisasa ya mwendo Kasi(SGR).


Aidha wananchi hao walieleza kuwa eneo hilo Sasa limegeuka kisiwa kutokana na wao kukosa namna ya kupitia hasa kipindi inaponyesha mvua na kuongeza gharama kubwa za maisha.


Walizungumza hayo baada ya timu kutoka tume hiyo ya binadamu na utawala Bora kufika katika eneo hilo na kusikiliza malalamiko yao.


Baadhi ya wananchi walisema kuwa pamoja na kuwepo kwa treni ambayo imesaidia na kurahisisha usafiri kutoka Morogoro kwenda Dar es salaam kwa kiasi kikubwa waliomba Serikali kuwajengea kivuko cha juu(FLYOVER).


"Tunaipongeza Serikali imefanya kazi nzuri kwenye kujenga hii RELI na kutuletea treni lakini kuna tatizo la sisi tulioko upande wa pili hasa kwenye suala la barabara hakijazingatiwa ipasavyo,saivi tumekuwa kisiwani, mkandarasi ameavha mashimo makubwa, maisha yamekuwa ya gharama hata wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule,"alisema Joseph Msofe mkazi wa Yespa.


Kujengwa kwa kivuko cha juu kitasaidia wananchi wa eneo hilo kuingia na kutoka kwa urahisi wakati wote.


Naye meneja Yespa Sekondari,Yesse Mzava alisema katika kupitia kwa mradi wa mwendo kasi kumesahau kuweka miundombinu hasa barabara ya wananchi na kusababisha maisha kuwa magumu na barabara zilizowekwa ziko kwenye mkondo wa maji ambapo mvua inaponyesha wamekuwa wakishindwa kupitia.


Mzava alisema Serikali haikufatilia wakati wa itekelezaji wa mradi haukuzingatia hata taasisi zilisopo kama shule namna watakavyopata huduma na hiyo imesababisha wanafunzi kukosa kwenda shule kwa urahisi.


Mkazi mwingine wa Yespa Grace Chilongola alisema huduma mbalimbali hazipatikani kama zahanati, kituo cha Polisi ambapo kwa Sasa ikitokea mgonjwa kupata huduma ya haraka inakuwa vigumu jambo ambalo linaweza sababisha vifo vizivyokuwa vya lazima.


Abel Isaya,mwekezaji mradi wa kuku uliopo eneo la Yespa alisema kwa sasa wamekuwa na wakati mgumu kutoa huduma na hata mizigo yao kuharibisha kwa kupata hasara kubwa, ambapo aliiomba Serikali kutengeneza barabara.


"Badala ya kuzalisha kwa sasa kilichobaki ni kupata hasara na kuomba Serikali kuangalia kwa jicho la huruma jambo ambalo litapelekea mradi kufingwa na watu kukosa ajira na hata kukosekana kwa ulipqji Kodi,"alisema.


Wakati huo huo, wananchi hao walitaka hatma ya shimo lililochimbwa na mwekezaji baada ya kumaliza ujenzi wa mradi wa SGR pamoja na viwanja vilivyopita kwenye makazi.


Mkurugenzi wa huduma za kisheria,tume ya haki za binadamu na utawala bora Nabo Assey, alisema wamepokea malalamiko ya wananchi hao na kwamba yatafanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na mengine kupelekwa kwenye Wizara za kisekta.


Assey alisema wamekuja Morogoro kwa ajili ya Kukusanya maoni ili kuandaa mpango kazi wa kitaifa kuhusu masuala ya haki za binadamu na biashara ambapo alizungumzia changamoto walizopokea kuwa tume kama taasisi wataziainisha kwenye mpango kazi ili ziweze kuonekana ili inapoandaliwa miradi mbalimbali masuala yaweze kuzingatiwa.


Mkurugenzi huyo alisema kilichoonekana ni Mamlaka za serikali kutokuwepo kwa mawasiliano pindi miradi inapofanyika na kwamba watatumia mpango kazi huo kupatikana kwa suluhisho.


"Tume inaeleza kuwa watu wote Wana Hali, lakini tunachokiona ni ushirikishaji kwa wananchi kwenye miradi mbalimbali unatakiwa,"alisema.


mwenyekiti wa mtaa wa Yespa Rukia Gunda,alisema alimshukuru kupatikana kwa reli ya mwendo Kasi pamoja na kuwepo kwa changamoto ya vivuko wananchi kushindwa kupitia kutokana na maji mengi yanayopita kwenye barabara za chini zilizopo na kulazimika wananchi kutembea kwa miguu na kutumia pikipiki ama baiskeri kwenda makazini.


Mwisho.

No comments: