Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa kulia akimkabidhi jiko la Gesi mmoja wa wanufaika |
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa kulia akimkabidhi mmoja wa wanufaika wa majikonhayo |
Na Mwandishi wetu,Namtumbo
maipacarusha20@gmail.com
MAJIKO ya nishati mbadala 300 yenye thamani ya sh 25.5 milioni yametolewa kwa wajasiriamali wadogo wanaotoa huduma ya chakula Mama na Baba lishe Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa amesema kutolewa kwa majiko hayo ni ili waweze kutumia nishati safi na kuondokana na ugonjwa wa kukosa pumzi na vifo vinavyotokana na kuvuta moshi wenye sumu
Akizungumza na wajasiliamali hao jana wakati wa hafla fupi ya ugawaji wa majiko hayo ambayo ni msaada kutoka kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan mbunge Kawawa alisema wabunge kila mara wamekuwa wakipiga kelele ya kuomba bei ya gesi kushuka ili kila mwananchi aweze kutumia nishati safi na Salama ya kupikia na kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ORYX Peter Ndomba alisema kila mwaka watu 33,000 ufariki dunia kutokana na kuvuta moshi wenye sumu hivyo aliwashauri wananchi kutumia nishati safi ya kupikia kwa ajili ya afya zao.
Nao Wajasiriamali hao akiwemo Tugonze Pawa na Sophia Hamis walisema kuwa wamepokea majiko hayo lakini ombi lao kubwa kwa serikali ni kupunguzwa kwa gharama za ujazaji wa gasi ili iendelee kuwa msaada kwao .
Mwisho.
No comments:
Post a Comment