Mwanafunzi atwaa ubingwa mbio za baiskeli Tanga. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 13 July 2024

Mwanafunzi atwaa ubingwa mbio za baiskeli Tanga.

 

Omari Idd akiwa ameshikilia baiskeli baada ya kuibuka bingwa wa mashindano ya mbio za baiskeli kuadhimisha mwaka wa kiislamu wa 1446 zilizoandaliwa na Masjid Noor Kange kwa kushirikiana na Chama cha mbio za baiskeli Mkoa wa Tanga.

Kiongozi wa Noor Masjid wa Kange jijini Tanga akimkabidhi zawadi Omar Idd baada ya kuibuka bingwa wa mbio za baiskeli kuadhimisha mwaka wa kiislamu 1446 zilizoandaliwa na Chama cha mbio za baiskeli Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Masjid Noor Kange.

Pichani ni washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli kuadhimisha mwaka wa kiislamu wa 1446 zilizoandaliwa na Masjid Noor Kange kwa kushirikiana na Chama cha mbio za baiskeli Mkoa wa Tanga nankufanyika Kange jijini Tanga


Na: Burhani Yakub, Tanga


maipacarusha20@gmail.com


Omari Idd ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kange ameibuka bingwa wa mbio za baiskeli za kuadhimisha mwaka mpya wa kiislamu wa 1446 zilizofanyika Kange jijini hapa.

 

Omari aliweza kumaliza mbio hizo zilizoanfaliwa na Masjid Noor Kange za kilomita 15 kwa kutumia saa 1;53;30 akifuatiwa na Adam Abdul aliyekimbia kwa saa 1;53;33 huku Athumani Azizi akishika nafasi ya tatu kwa kukimbia kwa saa 1;53;40.

 

Nafasi ya nne ilikwenda kwa Issa Rashid aliyekimbia kwa saa 1;54;00  ambapo Amani Hussein alimaliza akiwa nafasi ya tano akitumia saa 1;54;20 akifuatiwa na Athumani Imma,Idrisa Mussa,Nasri Gama,Muhud Mutwalib Abdul Aziz  na Ally Rashid.

 

Katibu wa Masjid Noor , Juma Nyange alisema lengo la mashano hayo ni kukuza vipaji vya vijana katika michezo na kuadhimisha mwaka mpya kwa kiislamu.

 

“Kwa kushirikiana na chama cha mbio za baiskeli mkoa wa Tanga tumeazimia kuboresha zaidi mchezo huu kwa mwaka ujao ambapo tutapanua kwa kushirikisha vijana bla kubagua dini zao,tutaongeza kilomita na zawadi zitakuwa kubwa zaidi “alisema Nyange.

 

Katibu wa Chama cha mbio za Baiskeli Mkoa wa Tanga,Muzamilu Mafita aliahidi kutoa  ushirikiano wa hali na mali katika mashindano hayo kwa kuwa yanasaidia kuhamasisha na kuhuisha mchezo huo ambao ni ajira kubwa kwa vijana.

 

“Mbio za baiskeli ni mchezo ambao umekuwa ukiwawezesha vijana kupata fursa ya kwenda nchi mbalimbali Duniani kushiriki mbio hizo kwa hivyo tuna kila sababu ya kuwaandaa wakiwa wadogo”alisema Mafita.

 

No comments: