SERIKALI KUGAWA MITUNGI YA GESI YA BILIONI 10 KWA WANANCHI MBINGA ILI KUZUIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 25 July 2024

SERIKALI KUGAWA MITUNGI YA GESI YA BILIONI 10 KWA WANANCHI MBINGA ILI KUZUIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

 





Na Mwandishi wetu Mbinga


maipacarusha20@gmail.com


Serikali imepanga kutoa mitungi ya gesi 452,445 yenye thamani ya Shilingi bilioni 10 kwa wananchi  ili kuzuia uharibifu wa mazingira


Aidha Serikali imeweka mikakati ya kuongeza matumizi ya gesi ya kupikia na kupitia REA imeshatoa mitungi ya Ruzuku elfu 83,500 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.5 na mwaka huu wa fedha .


Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga Alisema hayo wilayani Mbinga wakati akizungumza na wananchi katika hafla ya ugawaji wa mitungi ya majiko ya gesi ORYX  wilayani humo.


 Kapinga alisema kuwa matumizi ya gesi hii yanachukuliwa kwa umhimu mkubwa kutokana na aina ya kipekee ya gesi hiyo,nishati hiyo ni safi na salama hususani gesi ya ORYX ukilinganisha na nishati zingine kama mkaa na kuni.


Awali Mkurugenzi Mkuu wa ORYX Benoit Araman alisema kuwa watanzania elfu thelathini  na tatu  hupoteza maisha kila mwaka  kwa kuvuta moshi na chembechembe  zitokanazo na mkaa na kuni lakini kwa kutumia na kupikia gesi ya ORYX kutatatua jambo hilo.


Araman  alisema ulinzi wa mazingira  kupika kwa kutumia gesi ya ORYX kutazuia ukataji wa miti,kwa hiyo itasaidia kulinda mazingira yetu na ukitumia gesi hii utapika kwa haraka na kwa ufanisi na wananwake wengi watakuwa na muda wa kufanya kazi za kijami,maendeleo ya kijamii na maendeleo yao binafsi.

 

Alisema kuwa ubora wa hali ya maisha  kupika kwa kutumia gesi ya ORYX  huzui wanawake kutumia masaa mengi ya kazi kwa kukusanya kuni misituni na kukutana na wanyama pori pamoja na majanga mengine.


Naye Celina Mbunda mkazi wa Mbinga  alimshukuru Naibu waziri  kwa kutoa mitungi ya gesi kwwni itawarahisishia kupika kwa haraka  na kuweza kupunguza adha kutumia kero.


Mwisho.

No comments: