WAZIRI AWESO AAGIZA BODI YA MORUWASA KUMSIMAMISHA KAZI MTAALAMU WA UFUNDI, BONDE WAMI RUVU NA MORUWASA KUDHIBITI MAGUGU BWAWA LA MINDU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 23 July 2024

WAZIRI AWESO AAGIZA BODI YA MORUWASA KUMSIMAMISHA KAZI MTAALAMU WA UFUNDI, BONDE WAMI RUVU NA MORUWASA KUDHIBITI MAGUGU BWAWA LA MINDU

 





Na: Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com 


WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza Bodi ya Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingira (MORUWASA) kumsimamisha kazi mtaalamu kiongozi wa ufundi mhandisi Thomas Ngulika kwa tuhuma za kuihujumu Mamlaka hiyo na kusababisha baadhi ya maeneo Manispaa ya Morogoro kukosa maji kwa zaidi ya wiki tatu.


Waziri Aweso alitoa agizo hilo katika ziara yake ya siku Moja, ambapo katika kikao chake na watumishi, menejimenti na Bodi ya Mamlaka hiyo ya Moruwasa baada ya kutembelea na kukagua Hali ya upatikanaji maji katika bwawa la Mindu, kituo cha kuzalisha na kutibu maji cha Mafiga, na Mtambo wa kusukuma maji eneo la Tumbaku.


Katika kikao hicho Waziri Aweso alisema amebaini kuwepo kwa hujuma kwa mamlaka hiyo zinazofanywa na baadhi ya wafanyakazi, ikiwemo ya Mtaalamu kiongozi huyo wa ufundi unaofanywa makusudi kwa kushindwa kuwapatia maji wananchi wa kata za pembezoni ikiwemo eneo la nanenane kata ya Tungi kwa zaidi ya wiki tatu.


"Kwa wiki tatu mfululizo maeneo ya nanenane na tungi maji hayatoki na  mlipoona nakuja ndipo mkafungulia maji kwenye maeneo hayo, hii inaonekana ni hujuma kwa mamlaka,"alisema Waziri Aweso.


Aidha alisema Wizara haitavumilia na kutokuwa tayari kuona mtendaji wa mamlaka kwa makusudi anatoa taarifa za uongozi wakati yeye anahusika kuhujumu.


"Kazi ya kwanza kwa mtu wetu ambaye anayehusika na technical atupishe kwanza na Bodi ipo imsimamishe kazi mara Moja, na la pili naenda kwenye kikao Dodoma nitarudi na kuwasaidia lakini ipo timu yangu inanisaidia kufanyakazi, lazima Moruwasa itaenda tu na sisi watumishi tukafanya kazi na najua mna changamoto zetu nimeshazipata na tutazitatia na nazifanyia kazi,"alisema.


Pamoja na kutoa agizo, Waziri Aweso katika uchunguzi weke mfupi alibaini mambo kadhaa ikiwemo Menejimenti kutokuwa pamoja kila mtu ana jambo lake, watumishi wa chini kutosimamiwa kupata stahiki zao kwamba watumishi Wanafanya kazi na hawana molari na kwamba haiwezekani kuwepo kwa mamlaka yenye makundi.


"Hatuwezi kuwa na taasisi ya namna hiyo ya makundi na watumushi wa ngazi ya chini hawapati stahiki zao kwani na wao watajitengenezea uhalali wa kupata fedha kwa wananchi, na baadhi watumishi wameunda Mamlaka zao,"alisema.


Katika hatua nyingine Waziri Aweso ameziagiza Mamlaka za MORUWASA na Bonde la Wami Ruvu (WRBWB)kudhibiti Magugu maji yaliyoota katika bwawa la Mindu.


Aidha Waziri Aweso aliahidi Serikali kuharakisha mchakato wa fidia kwa wananchi ambao makazi yao yalihakukiwa na kupaswa kulipwa  waliopo pembezoni mwa bwawa hilo ili waondoke haraka na kupisha shughuli za uhifafhi na uendelezaji wa bwawa.


Waziri Aweso alizitaka Mamlaka hizo kuweka nguvu kwenye suala zima la kulinda na kutunza ikiwa ni pamoja na kudhibiti  kwa kushirikiana na wananchi kwani Bwawa la Mindu ndio roho ya Wana Morogoro.


"Shirikianane kuhakikisha eneo la bwawa la mindu linakuwa kwenye mazingira sawa kwa kutimiza wajibu wao, Pakiteteleka Mindu maana mnawaweka watu kwenye mtihani, pili tunaona makazi ya watu yanazidi kusogea katika chanzo hiki Kikuu nafikiri tuwashirikishe viongozi wa maeneo haya kwa sababu jamii hipo ili tusikwame,"alisema.


"Na huu ni muda muafaka wa wale walifanyiwa tathimini wakapisha maeneo na Sisi Wizara tutazingatia suala la kulipa fidia,"alisema Waziri huyo wa Maji.


Awali akizungumza mbele ya Waziri Aweso, Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA mhandisi Tamim Katakweba alieleza mipango waliyo nayo kama Mamlaka ambapo moja ya mpango ni kunyanyua tuta la bwawa la Mindu ambalo ni chanzo kikuu cha maji kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro na mikakati zaidi ya kupongeza uzalishaji.


Mhandisi Katakweba alisema tuta hilo litanyanyuliwa kwa mita 2.5 ili kukikwa kwa maji yaliyokuwa yakimwagika yaweze kurudi kwenye bwawa.


Akiwa mjini Morogoro Waziri Aweso amekagua shughuli za Mtambo wa kusukuma maji eneo la Tumbaku, kuonana na wateja wa maji katika kiwanda cha kuzalisha nguo Cha 21st Century na nanenane unapofanyika uchimbaji wa kisima.




No comments: