Maeneo ya Urithi wa Dunia Yanachangia Kukuza Utalii - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 23 July 2024

Maeneo ya Urithi wa Dunia Yanachangia Kukuza Utalii

 





Na: Mwandishi Wetu, New Delhi


maipacarusha20@gmail.com


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesema sekta ya utalii nchini Tanzania inaendelea kufanya vyema ikichangiwa pia na utunzaji wa malikale na maeneo mengine ya urithi wa Dunia.


Dkt. Abbasi ameyasema hayo katika mahojiano aliyoyafanya leo Julai 23, 2024 wakati wa Mkutano wa 46 wa Kamati ya Maeneo ya Urithi wa Dunia chini ya UNESCO unaoendelea jijini Delhi ambapo miongoni mwa taarifa za uhifadhi (state of conservation reports) zitakazowasilishwa zipo zitakazogusa maeneo yaliyolindwa kama sehemu ya urithi wa dunia kama Serengeti, Ngorongoro, Nyerere/Selous na Mji Mkongwe wa Zanzibar. 


“Maeneo hayo yamekuwa na mchango mkubwa sana kukuza utalii kwa sababu yamekuwa moja ya vivutio tunavyovitegemea na tuko hapa kuonesha mshikamano na dunia nzima katika kuendelea kuweka nguvu za pamoja kuyahifadhi na kuyatangaza,” alisema Dkt. Abbasi akigusia kuwa takwimu za miezi sita (Januari-Juni, 2024) zinaonesha utalii umeongezeka kwa takribani asilimia 25 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2023. 


Mkutano huo pia unahudhuriwa na Waziri wa Utalii na Mambokale wa Zanzibar, Mhe. Mudrik Soraga na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa ambaye pia ni Mwakilishi wa Tanzania katika UNESCO, Balozi Ali Mwadini.

No comments: